Kuna umri ukifika kukaa kwa ndugu mwenye familia si uungwana hata kama ni kaka au dada, mpishe tafuta shughuli uende kwako!

Kuna umri ukifika kukaa kwa ndugu mwenye familia si uungwana hata kama ni kaka au dada, mpishe tafuta shughuli uende kwako!

R-K-O

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2023
Posts
482
Reaction score
2,178
Kuna umri unafika kwenda kwa ndugu iwe ni kwajili ya kumjulia hali unarudi kwako, umeenda mkoa wake kikazi kakuhost ukae kwake ukimaliza unarudi kwako, unaumwa kakupeleka kwake akuuguze ukipona tafta shughuli nenda kwako

Ndugu yako kashaanza maisha ya familia ni vema umpishe,

Haya ni mambo utahamishia huko na wanaweza wasikuambie ila jua uwepo wako ni mzigo.

Kuvuruga bajeti,

Kumchosha house girl

Watoto kubanana chumba kimoja ili ndugu walale vingine.

Privacy ndogo
 
Huwez pata michango ya hoja kwasabab 90% ya wanawake na wanaume na vijana wa humu JF wenye umri wa kujitegemea bado ni wavivu wajinga wanaishi kwa ndug zao na kwa wazaz wao wakitegemea kula na kulala bure bila kufanya kazi yoyote... Kazi yao kuzurura JF, twita, FB, IG na Wasap... Vipuuzi sana
 
Mnaokaa kwa ndugu zenu nawapongeza mna level kubwa ya ustahimilivu! Nlikaa wiki moja Kwa ndugu kipindi hiko nimetoka advance kwanza hutakiwi kuangalia mpira wanasema ni dhambi😁😁

Jioni mnasali sana ndefu kinyama yaani mnasali pamoja then moja anaconclude dadeq siku hyo wakanipoint niconclude nikapiga kitu Cha baba yetu uliye mbinguni ......

Hamna kucheza pool table dadeq
 
Huwez pata michango ya hoja kwasabab 90% ya wanawake na wanaume na vijana wa humu JF wenye umri wa kujitegemea bado ni wavivu wajinga wanaishi kwa ndug zao na kwa wazaz wao wakitegemea kula na kulala bure bila kufanya kazi yoyote... Kazi yao kuzurura JF, twita, FB, IG na Wasap... Vipuuzi sana
Hv hao wanaoshindia kwa ndugu Hela ya bando wanapataga wapi?
 
Kukaa Kwa Ndugu ni vipindi
Ipo siku yule anae Kwa Ndugu atasepa atajitegemea kivyake
Ishu ni Kukaza na awe na Determination
Awe mvumilivu wa Kwa Hali yoyote ile.
Atakua mzuri siku Moja.
Nimewahi kukaa Kwa Ndugu miaka zaidi ya 7
Panahitaji uvumilie na ukumbke pale sio Kwenu.
 
Back
Top Bottom