Kuna umuhimu kwa Msigwa wa Ikulu kuangalia upya utaratibu wake wa kuongoza hafla za Rais

Kuna umuhimu kwa Msigwa wa Ikulu kuangalia upya utaratibu wake wa kuongoza hafla za Rais

Bulesi

Platinum Member
Joined
May 14, 2008
Posts
14,275
Reaction score
13,929
Nilihudhulia hafla ya kuapishwa kwa Mawaziri kule Ikulu ya Chamwino na nikaona jinsi press secretary Msigwa alivyoendesha lile zoezi la kuapishwa kwa mawaziri na Mheshimiwa Rais Samia.

Ni vizuri kuwapa nafasi viongozi wachache kutoa neno moja au mawili katika shuhuri kama hizo lakini sio kila mara na sio kila wakati kunapokuwepo na shuhuri za namna hiyo viongozi kama Spika , Waziri Mkuu, Jaji Mkuu na hasa hasa Makamu wa rais watoe hotuba.

Sometimes it becomes embarrassing kwa wahusika kwani watajikuta wanarudia maneno yale yale waliyosema siku mbili zilizopita kwenye hafla kama hiyo!!

Hafla yeyote inayomuhusu Rais, hiyo inakuwa nafasi yake yeye kuwa na platform ya kuzungumza na wananchi ;kama kuna kitu anataka kuwafahamisha.

Sio vizuri anapokuwepo Rais kumuomba makamu wake nae azungumze labda kwa yeye mwenyewe Rais kumtaka afanye hivyo. Hafla ya Rais ni platform yake ya kuzungumza, hao wengine yeye mwenyewe akitaka ataamuru hivyo.

RAIS NDIO MWENYE KUTOA NASAHA ZAKE KWENYE HIZO PLATFORMS. REMEMBER HAO WENGINE ARE SERVING AT HER PLEASURE!

Kumbuka Msigwa, enzi ya mwendazake hata siku moja sikumsikia makamu wake akitoa hotuba kabla yake hivyo usibadili utaratibu watu watakutafsiri sivyo na unga unaweza kumwagika!!
 
Msigwa anasema, "Mheshimiwa Rais, kwa ruhusa yako naomba Makamu Wa Rais aongee kidogo" kabla ruhusa haijatolewa, tayari Makamu anaanza kuongea na kutoa maagizo makali.

Msigwa tena, "Mheshimiwa Rais hapa navunja protokali kidogo, kwa ruhusa yako nimuombe Katibu Mkuu Kiongozi kuongea". Kabla ruhusa ya kuvunja protokali kutolewa au ruhusa ya KMK kuongea, tayari KMK anaongea.

Ni kama Ratiba inakuwa haioneshi nafasi ya hao watu kuongea ila Msigwa anapanga ratiba isiyoandikwa.
 
Mimi nadhani ni wakubadilisha maana anauelekeo ule ule wa awamu ya tano, juzi ile alichapia kidogo wakati akimtaja mh rais kwa kwa kumuita mheshimiwa rais docter! akastuka akavunga.
 
Kuna wakati alisahau kumtambulisha makamu wa rais mh mpango! So sad!
 
Hujawahi kumsikia mama Samia akitoa hutuba kipindi Cha JPM? Huu uongo mnasomea au mnarithi?
Kwa jiwe mwenyewe kumuomba kutoa neno !! Sio kwa msigwa kumuomba rais awaite kuzungumza! Kuna tofauti kubwa.
 
Naona mnamsagia Msigwa kunguni tuu..

Mwenzetu amefanikiwa,ana uelewa na kazi yake na ndio maana amefika alipo..

Kuwa (DPC) Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu sio kitoto.

Cha muhimu tupambane kutafuta ugali mambo ya protocol huwa yanavunjwa eneo lolote na wakati wowote haijalishi ni hafla za Raisi au kiongozi yeyote.

Cha mwisho hata hao waliovunjiwa protocol na kupewa nafasi hawajatukani mtu
 
mimi nadhani ni wakubadilisha maana anauelekeo ule ule wa awamu ya tano, juzi ile alichapia kidogo wakati akimtaja mh rais kwa kwa kumuita mheshimiwa rais docter! akastuka akavunga

Zamani alikuwa hafanyi hivyo kuita anavyotaka yeye ila sasa kazidi
Yaani anaomba huku tayari imekuwa kama amri hajamaliza na mtu kaisha amka
 
Hujawahi kumsikia mama Samia akitoa hutuba kipindi Cha JPM? Huu uongo mnasomea au mnarithi?
Alichoandika na nilichomwelewa mleta mada, hao wanaokaribishwa, wanapaswa kupewa nafasi na Rais mwenyewe. Press za Magufuli, akina Samia na Majaliwa walikuwa wanapewa nafasi na Magufuli mwenyewe(kwa zile nilizoangaliwa, huenda kwa zile ambazo sikuangalia, walioaribishwa na Msigwa).
 
Ulichpost hapa ni uelewa wako duni! Anachokiongoza Msigwa huwa kimeshapitiwa hadi na Rais! Wewe kama ulihudhuria hiyo sherehe basi ni bahati yako maana hata neno HUDHURIA umeandika HUDHULIA, sasa nina wasiwasi kama una umaarufu wa kuwepo pale kwa uandishi wako hafifu!
 
mimi nadhani ni wakubadilisha maana anauelekeo ule ule wa awamu ya tano, juzi ile alichapia kidogo wakati akimtaja mh rais kwa kwa kumuita mheshimiwa rais docter! akastuka akavunga
Kwa sababu hiyo ndio abadilishwe,au mumesahau kuwa nae Samia alikuwa ni mmojawapo wa hii timu manyotaka isafiswe,tumekuwa watu wa ajabu sana.
 
Kwa sababu hiyo ndio abadilishwe,au mumesahau kuwa nae Samia alikuwa ni mmojawapo wa hii timu manyotaka isafiswe,tumekuwa watu wa ajabu sana.
Yaani shida tupu!

Msigwa anatafutwa vibaya mno! Sijui huyu DPC kawakosea nini hawa binadamu.

Jamaa anatafuta kaugali chake na watoto wake waishi.. maisha yaende bado anasagiwa kunguni.

Abasi + Msigwa sio wanasiasa....wanafanyia kazi taaluma zao.
 
Awekwe Jokate atafaa. Zamu ya Kisura sasa. Huyu mwenye sauti baya apishe wengine sasa.
 
Back
Top Bottom