Mara zote wapiga kura huchagua mtu na wala sio chama.
Chama chochote kinaweza kuwaomba wapiga kura wachague chama badala ya mtu. Kwa kuzingatia, hilo haliwezekani, na likiwezekana litakuwa ni kwa kuzingatia propaganda iliyofanywa tu. Sababu ni kama zifuatazo:
1. Wagombea wote ni watu na si vyama. Vyama huteua wagombea tu
2. Kampeni zote hufanywa na watu/wakijinadi uwezo wao na kutoa ahadi za kutimiza matarajio ya wapiga kura wao. Hutumia sera za vyama vyao ili kufanikisha malengo yao
3. Mshindi wa uchaguzi ni mtu. Mshindi hutangazwa dhidi ya walioshindana nae na mtangazaji ni Tume ya Taifa ya uchaguzi
4. Viapo vyote baada ya ushindi ufanywa na watu na wala sio vyama. Hakuna kiongozi wa chama anaesimamishwa ili kula kiapo kutokana na ushindi wa mwanachama wake
5. Uwakilishi wa mshindi (Diwani, Mbunge, n.k) hufanywa na mtu kwa kuzingatia vipaumbele vya watu ambao mtu huyo anawawakilisha. Hakuna chama kinachowakilisha watu
6. Chama kinafaidika kwa kupata support kutokana na ushindi wa mtu katika mabaraza ambayo mtu huyo amechaguliwa kuwa mjumbe (Council, Bunge, Baraza la Mapinduzi ZNZ).