Kuna umuhimu wa kufungua kesi mahakamu kuu kupinga mchakato huu "haramu" wa katiba mpya

Kuna umuhimu wa kufungua kesi mahakamu kuu kupinga mchakato huu "haramu" wa katiba mpya

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Mchakato huu wa kupata katiba mpya umegubikwa na dossari nyingi tangu hatua za awali kabisa ikiwa ni pamoja utungwaji wa sheria ya mabadiliko ya katiba.

Hoja za msingi zinazonifanya nione hata hii sheria ni haramu ni pamoja na vipengele kama:

1.Wabunge wa Bunge la Jamuhuru na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kujigeuza kuwa wajumbe halali wa Bunge maalumu la Katiba.

2.Raisi kuteua wajumbe wa Bunge la Katiba

3.Wajumbe wa Tume ya Katiba kuteuliwa na Raisi

5.Kutokuwepo kwa mkutano mkuu wa Taifa kuhusu katiba

6.Tume ya uchaguzi(tume isiyo huru) kusimamia kura ya maoni

7.Kuanza mchakato wa kupata katiba mpya kabla ya kuitisha kura ya maoni ili watanzania waamue hatima na muundo wa muungano.

Mbali na kasoro hizo za kisheria,kasoro zingine zinazoendelea kujitokeza ni pamoja na

1.Kwepo kwa rasimu zisizo rasimi

2.Kusambazwa kwa waraka usio rasimu(haramu) kutoka kwenye vyama vya siasa kwenda kwa wajumbe wa Bunge la Katiba ili kuwashawaishi wajumbe hao walinde maslahi ya vyama husika.

3.Vyama kuwa na misimamo na kuwataka wanachama wao kutetea msimamo wa chama badala ya wajumbe hao kutetea maslahi ya wananchi wao.

Mimi nina amini kwasababu hizo hapo juu,mchakato huu mzima ni haramu na wanasheria wanapaswa kufungua kesi mahakamu kuu au mahakama ya katiba kama ipo kupinga mchakato huu.

Ninajua kuna watu watakuja na hoja kuwa wazo hili limechelewa lakini mimi nawambia "better late than never".
 
Kesi ya Nyani unampelekea Ngedere!!?? Majaji wa Mahakama Kuu, ndiyo haohaoooooo! .... Presidential appointees! Mara hii umekwishasahau walivyofanya katika kesi ya msaliti "Nyepesi"?
 
Kesi ya Nyani unampelekea Ngedere!!?? Majaji wa Mahakama Kuu, ndiyo haohaoooooo! .... Presidential appointees! Mara hii umekwishasahau walivyofanya katika kesi ya msaliti "Nyepesi"?

Anyway,sijui tukimbilie wapi!
 
Back
Top Bottom