Salaam wakuu
Nina kesi ya madai ya talaka.
Mimi ndiyo mdai ba kesi imefikia hukumu. Ilipangwa hukumu iwe disemba, mdaiwa akaleta udhuru na ikapangwa jana alhamisi ambapo mdaiwa akaleta tena udhuru kuwa anaumwa. Sasa hukumu imepangwa iwe Februari. Swali langu
1. Ni lazima niwepo siku ya hukumu? Je naweza kuomba kuwakilishwa na jamaa yangu
2. Ni lazima mdaiwa awepo siku ya hukumu?
3. Kwa kuwa naamini hakimu anayo maamuzi tayari, je kutokufika kwangu kunaweza kubadili maamuzi hayo?
Karibuni kwa msaada