Kuna umuhimu wa serikali kufanya ukaguzi hizi shule binafsi. Watoto darasa la 4 wanawekwa Shuleni mpaka saa 12 jioni Jumatatu - Jumamosi

Mzalendo03

New Member
Joined
Feb 18, 2025
Posts
2
Reaction score
5
Shule moja inaitwa Center for Education Plus Darasa la 4 miaka 9 wanakalishwa shuleni mpaka saa 11 Jumatatu mpaka Jumamosi wanafika nyumbani saa 1 usiku.

Huyu mtoto anasoma nini?. Ubongo wake umeshakomaa kukaa muda wote huu akisoma?. Sio sawa kabisa.. Angalau wangefanya mara 3 kwa Wiki.

Na weekend mtoto anatakiwa apumzike na ajifunze vitu vingine vya Art. Maisha sio Geographia na Historia. Tanzania mpaka leo hawajifunzi tuu.

Wanakimbizana na Shule kufanya vizuri kwa kuwakremisha watoto. Ili wao wapige hela Matokeo yake mtoto akimaliza shule awezi kufanya vitu vingine na anakuwa sio mbunifu .
 
Umeandika ukweli tatizo siasa sana kila sehem. Ayo mavgeography ata apate A kwa kukremishwa hayana nsaada wowote kwa life yake labda kuanza kulilia ajira za ualimu tena baadae.
 
Sio shule binafsi pekee. Nimeona shule za serikali pia za msingi mtoto anakaa muda mrefu shuleni mpaka saa kumi na Moja jioni. Hii sio sawa kwa afya ya mtoto
 
Darasa la nne na la Saba yote ni madarasa ya mitihani. Sasa wakiachwa wakifeli, mnaanza kulaumu.
Lakini pia kwani umeambiwa huo muda wote wanakuwa wanasoma? Hakuna break? Hakuna Kula? Hakuna kupumua Kidogo?

Huko nyumbani wanakoshinda na katoon siku nzima, huoni madhara yake?

Acheni wapigwe drills za kutosha. After all sio Kila mwaka, ni Kwa mwaka wa mitihani ya kitaifa inayoamua mustakabali Yao tu.
 
Mijitu myeusi haielewi nini maana ya elimu na njia sahihi ya kufikisha hiyo elimu.

Elimu imekuwa biashara.Wazazi wengi ni vilaza hawajui chochote kuhusu elimu wao wanachojua ni kulipa ada.Mtoto apate dividion 1 akawatambie majirani na ndugu zake😀😀😀.

Hii furaha ya bandia kufurahia matokeo huwa inawapofusha wazazi wengi kiasi kwamba hawaelewi ni ipi njia sahihi watoto wao wapitie kuipata elimu ya kweli.

Taifa mufilisi kama hili ambalo raia hawajui hata vitu vya msingi(MAZOMBIE) kila kitu wanataka serikali ndo ifanye ni hatari kwa mstakabali wa maendeleo.
 
Kichwa cha habari hadi saa 12 ndani kwenye utumbo hadi saa 11 what is which sasa
 
1.Shule ziko kwenye mashindano ya kushika kumi bora kiwilaya, kimkoa na kitaifa.
kwa gharama kubwa ya muda wa watoto na fedha kwa wazazi.
Kuna shule mtoto anatakiwa afike saa 12 asb mpaka saa moja usiku! Jtatu - Jmosi.
Wazazi wana gharama ya kuwapeleka watoto muda huo na kuwachukua.

2.Shule nyingi zinaweka muda mbaya wa kuanza masomo na kumaliza ili kukulazimisha umpeleke mtoto boarding.
.Kumbuka boarding nayo ina gharama zake
 
Shule moja inaitwa Center for Education Plus Darasa la 4 miaka 9 wanakalishwa shuleni mpaka saa 11 Jumatatu mpaka Jumamosi wanafika nyumbani saa 1 usiku.

Huyu mtoto anasoma nini?. Ubongo wake umeshakomaa kukaa muda wote huu akisoma?. Sio sawa kabisa.. Angalau wangefanya mara 3 kwa Wiki.

Na weekend mtoto anatakiwa apumzike na ajifunze vitu vingine vya Art. Maisha sio Geographia na Historia. Tanzania mpaka leo hawajifunzi tuu.

Wanakimbizana na Shule kufanya vizuri kwa kuwakremisha watoto. Ili wao wapige hela Matokeo yake mtoto akimaliza shule awezi kufanya vitu vingine na anakuwa sio mbunifu .
Kama hutaki mpeleke mwañao kayumba,kwani ñyie ndio wadekeza watoto kama mayai mwisho wa siku mnatuangulia watoto machawa.
 
1.Shule ziko kwenye mashindano ya kushika kumi bora kiwilaya, kimkoa na kitaifa.
kwa gharama kubwa ya muda wa watoto na fedha kwa wazazi.
Kuna shule mtoto anatakiwa afike saa 12 asb mpaka saa moja usiku! Jtatu - Jmosi.
Wazazi wana gharama ya kuwapeleka watoto muda huo na kuwachukua.

2.Shule nyingi zinaweka muda mbaya wa kuanza masomo na kumaliza ili kukulazimisha umpeleke mtoto boarding.
.Kumbuka boarding nayo ina gharama zake

Middleincome/ paid slaves( Maskini waliochangamka) watoto zao ni mateka wa wafanyabiashara wa EMS.

📌Majambazi yameivamia elimu.
 
Darasa la nne na la Saba yote ni madarasa ya mitihani. Sasa wakiachwa wakifeli, mnaanza kulaumu.
Lakini pia kwani umeambiwa huo muda wote wanakuwa wanasoma? Hakuna break? Hakuna Kula? Hakuna kupumua Kidogo?

Huko nyumbani wanakoshinda na katoon siku nzima, huoni madhara yake?

Acheni wapigwe drills za kutosha. After all sio Kila mwaka, ni Kwa mwaka wa mitihani ya kitaifa inayoamua mustakabali Yao tu.
Issue sio kufaulu , Mnabidi muelewe na Afya ya Ubongo wa Watoto. Darasa la nne mtoto bado ni mdogo, angalau wangekuwa wanafanya mara 3 kwa wiki. Angalieni Shule za Singapor ama China . uwone kama watoto wa umri uwo wanasomeshwa masaa 12 shuleni

Mtoto anaitaji kukua na kucheza pia. NYie Sijuwi Ni walimu mnabidi mfundishwe na sayansi ya Ubongo . Awo watoto matokeo yake wanafaulu tuu Mitiani kwa kuwa mnawa kremisha. wakija kuingia mtaani hawana lolote.
 
Back
Top Bottom