SoC04 Kuna umuhimu wa taifa letu Tanzania kuweka malengo ya Mkoa ( Kimkoa)

SoC04 Kuna umuhimu wa taifa letu Tanzania kuweka malengo ya Mkoa ( Kimkoa)

Tanzania Tuitakayo competition threads

robbyr

Senior Member
Joined
Apr 8, 2017
Posts
129
Reaction score
221
Kwa nini tunahitaji malengo ya Mkoa?
3e79e46d42b082a92f95bbe67cdfa724.jpg

[ Picha: Pinterest]

1.Kutokuwa na usawa wa kimaendeleo, ukitazama tuna miaka sitini na ya uhuru wa taifa letu Tanzania lakini kuna maeneo bado huduma za maji hamna, afya ni shida, barabara ni taabu, elimu nayo shida lakini mengine yana neemeka kila siku na huduma hizo.

2. Mabadiliko ya viongozi mara kwa mara. Kutokana na mabadiliko ya viongozi wa mkoa na wilaya nimeona kuwa kila mkoa ni muhimu kuwa na malengo yake ambayo pia yataakisi yale ya taifa kwa ujumla mbali na ya ilani ya vyama vyetu vya siasa. Hii itasaidia viongozi kutokuongoza kwa matakwa yao bali kutimiza yale mtangulizi atakayo kuwa ameacha.

3. Utofauti wa kimaeneo, kila mkoa una Shughuli kubwa moja ya kiuchumi mfano Arusha na Kilimanjaro Utalii, na mingine Kilimo cha mazao na hata mambao. Hivyo, kuweka malengo ya kimkoa yatasaidia kuinua kila mkoa kwa nafasi yake kwa kupanga malengo kulinga na uhitaji.

4. Uwezo wa kifedha kama taifa, kulingana na pata letu la taifa ambalo hufanya bajeti kuwa finyu katika kuleta maendeleo ya haraka hivyo kuwema malengo ya kimkoa yatasaidia kuonesha maeneo gani yanahitaji uwezeshwaji au bajeti kubwa na hii itasaidia kutatua changamoto nyingi kwa muda mfupi.

Sababu zipo nyingi ila nataka nionyeshe kwa picha kidogo ni wapi malengo haya yanaweza kuwekwa.
Mfano:
a) Elimu, serikali inaweza kutazama kila mkoa na uhitaji wake kielimu na kuagiza viongozi kuweka malengo ya miaka mitano kwa kuainisha mambo gani yanahitajika kwenye elimu ikiwemo miundo mbinu, walimu, na zaidi pia wainishe kwa miaka mitano baadhi ya malengo yatafikiwa vipi. Kwani kuna maeneo yanahitaji nguvu zaidi tofautii na mengine.

b)Afya, malengo hayo yalenge pia kila mkoa na wilaya zake uanishe malengo ya kiafya hasa katika ujenzi wa hospitali na zahanati. Mfano mkoa wa Kilimanjaro umejaliwa sana vituo wa afya binafsi vingi tofauti na mikoa mingine hivyo mkoa unaweza kuweka pia malengo ya kuinua vituo hivyo viwe bora katika kutoa huduma nzuri lakini mikoa mingine inahitaji ujenzi wa vitua, vifaa, na hata watendaji. Kuweka malengo kutasaidia kutatua kwa mpangilio.

c) Kilimo, utoaji wa ruzuku, elimu, ili kilimo kiweze kuleta tija lazima mkoa uwe na picha kamili ya namna gani itaboresha kwa kila eneo la mkoa wake ambapo itasaidia kuakisi dira ya taifa vizuri na kuongeza uzalishaji kwa ajili ya matumizi ya ndani na nje ya nchi.


d) Makazi, kuna maeneo makazi ni duni sana kwani ni nyumba za udongo zenye paa la nyasi ambapo kipindi cha mvua huwa ni manyanyaso kwa wananchi. Kwa kuweka malengo ya mkoa kuna weza kusaidia hata kupunguza kodi kwenye saruji na vifaa vingine vya ujenzi kulingana na mkoa husika ili wakazi waweze kuwa na makazi bora.

Pia, barabara, umeme na maji, mfano kuna mikoa mpaka leo hawana matumaini ya kupata maji ila kungekuwa na malengo ya mkoa ingekuwa rahisi hata wilaya na maeneo ya ndani kufikika kwa urahisi na kubaini shida husika na namna ya kutatua kwa kufuata malengo ya mkoa huo.

Hivyo basi, ili kufanikisha malengo ya taifa basi lazima kuweka pembeni ilani ya chama na baada ya kupata malengo ya taifa itakuwa rahisi kubaini na kuweka ya mkoa na baadae katika utendaji tutapata matokeo imara.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom