Highlander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 3,093
- 1,075
Wadau hii changamoto ina maana gani kwetu raia?
Kuna kiasi cha maafisa wa polisi 38,850 katika jeshi la polisi la Tanzania, ambao ni kiasi cha afisa mmoja wa polisi kwa kila watu 1,150. Maafisa wa ziada 3,000 wako katika mafunzo huko Chuo cha Polisi Moshi katika mkoa wa Kilimanjaro, lakini jeshi linahitaji maafisa 48,011 zaidi kudhibiti idadi ya watu ya Tanzania ambayo ni takriban watu milioni 45.
Idadi hii ni pungufu ya nusu ya maafisa wanaohitajika kufikisha uwiano wa kimataifa unaokubalika wa afisa mmoja wa polisi kwa kila raia 400 hadi 500, kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Pereira Ame Silima bungeni.
Silima alisema jeshi la polisi Tanzania limeongezeka kutoka maafisa 28,000 mwaka 2006 hadi 38,000 mwaka 2012. Alisema ofisi yake itafanyia kazi upanuaji wa jeshi la polisi kwa kiwango cha asilimia 8.6 kwa mwaka, ikitegemea upatikanaji wa fedha. Silima pia alisema kuwa atafanyia kazi mipango ya kuongeza uwakilishi wa wanawake katika jeshi hilo, ambao kwa sasa ni asilimia 19, au maafisa wanawake 7,450 wanawake.
Source: Polisi ya Tanzania ina upungufu wa maafisa 48,000 - Sabahionline.com