Kuna upungufu wa Polisi 48,011 Tanzania

Highlander

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2012
Posts
3,093
Reaction score
1,075
Wadau hii changamoto ina maana gani kwetu raia?

Kuna kiasi cha maafisa wa polisi 38,850 katika jeshi la polisi la Tanzania, ambao ni kiasi cha afisa mmoja wa polisi kwa kila watu 1,150. Maafisa wa ziada 3,000 wako katika mafunzo huko Chuo cha Polisi Moshi katika mkoa wa Kilimanjaro, lakini jeshi linahitaji maafisa 48,011 zaidi kudhibiti idadi ya watu ya Tanzania ambayo ni takriban watu milioni 45.

Idadi hii ni pungufu ya nusu ya maafisa wanaohitajika kufikisha uwiano wa kimataifa unaokubalika wa afisa mmoja wa polisi kwa kila raia 400 hadi 500, kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Pereira Ame Silima bungeni.

Silima alisema jeshi la polisi Tanzania limeongezeka kutoka maafisa 28,000 mwaka 2006 hadi 38,000 mwaka 2012. Alisema ofisi yake itafanyia kazi upanuaji wa jeshi la polisi kwa kiwango cha asilimia 8.6 kwa mwaka, ikitegemea upatikanaji wa fedha. Silima pia alisema kuwa atafanyia kazi mipango ya kuongeza uwakilishi wa wanawake katika jeshi hilo, ambao kwa sasa ni asilimia 19, au maafisa wanawake 7,450 wanawake.


Source: Polisi ya Tanzania ina upungufu wa maafisa 48,000 - Sabahionline.com
 
Jeshi la Police ni bora tu lifutwe kwani hatuoni umuhimu wake.Sungusungu,jwtz na mgambo wanatosha.
 
Bora hata wasiongezwe kwa sababu
1. Serikali itawalipa nini kama hao tu waliopo inashindwa kukidhi mahitaj yao.
2. Watatumaliza bure maana siku hiz wanaua raia.
 
Jeshi la Police ni bora tu lifutwe kwani hatuoni umuhimu wake.Sungusungu,jwtz na mgambo wanatosha.

Bora hata wasiongezwe kwa sababu
1. Serikali itawalipa nini kama hao tu waliopo inashindwa kukidhi mahitaj yao.
2. Watatumaliza bure maana siku hiz wanaua raia.

Nikiri kujua Polisi hawapendwi sana Tanzania. Mazuri wanayofanya karibu yoote yanamezwa na msitu wa uhuni wanafanya. Sijui kama tutafika kweli tunakotaka kwenda. Na hizi takwimu si nzuri hata nashangaa Naibu Waziri aliziweka wazi hivi; huku ni kuwaambia raia police wapo out-numbered vibaya mno....

Uwepo wa Polisi hapa nchini ni katika mawazo tu, na si katika uhalisia wa kitakwimu.
 


Mazuri yapi wanayofanya? au kung'oa meno ya watu nakucha ndo mazuri
 
hao waliopo mnashindwa kuwaboreshea maslai yao sasa hao wapya mtawapa nini? au watakua mtawajengea mabweni waishi humo?
 
hao waliopo mnashindwa kuwaboreshea maslai yao sasa hao wapya mtawapa nini? au watakua mtawajengea mabweni waishi humo?

Mwenzangu?! Sijui....labda Silima atakuwa na jibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…