DOKEZO Kuna utapeli unafanyika Bayport Financial Service, unakopa kwao lakini mpaka makato ya kwanza yanafanyika mkopo uliyoomba haujakufikia!

DOKEZO Kuna utapeli unafanyika Bayport Financial Service, unakopa kwao lakini mpaka makato ya kwanza yanafanyika mkopo uliyoomba haujakufikia!

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mim ni mmoja wa wahanga katika kukopa mkopo katika taasisi ya fedha ya kukopesha inayoitwa Bayport Financial Service ambapo ni mwezi sasa toka nilipoomba mkopo mpaka rejesho la kwanza limefanyika ila hawajaweza kutoa huo mkopo.

Sasa ni kitu kinachoshangaza sana na kitu kama hicho ni kama utapeli tu haiwezekani umkate mtu mkopo hali ya kuwa hujampa mkopo na mamlaka husika kama BoT kulikalia kimya hili suala wakati ni kinyume na taratibu za huduma za fedha.
 
Hilo ni tatizo la payrol ofisi yenu ya utawala,wanapokeaje makato na kuwasilisha bila kuhakiki taarifa husika??

Tena kampuni yenyewe bayport au platnum,zina malalalmiko sana,sasa bado watapilitiza makato mwisho wa deni,na ofisi yako ina watu kazi kunywa chai tu na mikate.
 
Bayport ni kipengele malalamiko yamekuwa mengi si kwa wakopaji, si wafanyakazi wake.
 
Kausha damu hawa kuweni makini wamefilisi watu.
Siyo kufilisi tu bali hadi kuvunja ndoa za Watu kwa Ke kuliwa kimasihara na kuweka hati miliki za mali za Me bila ya Me kushirikishwa kabla ya kuchukua mkopo baada ya kuchemka rejesho la mikopo.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Hivi mpaka sasa mnaenda kukopa bayport hamjipendi kabisa majizi ya dunia nzima
 
Back
Top Bottom