Uchaguzi 2020 Kuna utaratibu gani wa kufuata kwa ajili ya kupiga kura kumchagua Rais katika kituo ambacho hujajiandikisha kwa huku Bara?

Igayo jr

Member
Joined
Jun 25, 2020
Posts
97
Reaction score
98
Habari!

Swali langu ni hilo, napenda kuelewa ni namna gani au sheria za Uchaguzi zinaruhusu kwa upande wa Bara kuweza kushiriki uchaguzi kwa kumchagua Rais katika kituo tofauti na nlichojiandikisha? Mwaka huu ni wa historia kwa nina jambo langu langu hapo baadae 28 Oktoba, kwa hiyo kwa mazingira yangu na si mimi tu wapo wengi wameniagiza kuuliza hili itakuwa vigumu sana kufika jimboni kwangu.

NB: Nashiriki kwa mara ya kwanza Uchaguzi huu kwa kupiga kura, hivo nahitaji mwongozo sahihi maana elimu ya mpiga kura hakuna kabisa huku mtaani.
 
Hakuna kitu kama hicho, mimi si msemaji wa NEC, lakini kwa matangazo waliyotoa kwenye vyombo vya habari, wanasema hakuna atakayeruhusiwa kupiga kura sehemu ambayo hakujiandikisha.
 
Uwezi kupiga kura ambapo hujajiandikisha! Kila kituo kinakuwa na orodha ya wapiga kura wahusika! Kama ulikuwa unajua utahama kituo ulipaswa kubadilisha taarifa kwenda kituo kipya unacho hitaji!

Watu wengi mnashangilia tuu lakini taratibu nyingi hamzijui na wala hamkuzifata ndio maana mkiambiwa kura zimeaibiwa mnakuwa wepesi kuamini!

Mtu awezi piga kura kama hayupo kwenye orodha ya hicho kituo..... na hiyo orodha hata mawakala hupewa!

Mnajua kushangilia lakini taratibu hamzijui na ndicho kitakacho wakuta wengi wenu
 
Mbona unajibu kwa jazba,
 
Maboresho ya daftari la mpiga kura yakishakamilika huwa hakuna namna nyingine tena
 
Usiseme hivo...kuna namna nyingi za kushiriki mchakato mzima wa uchaguzi mbali na kupiga kura mkuu.
 
Kura unapigia ulipojiandikishia tu kwa sharia za tume hii isiyikuwa huru nivo zilivyo
 
Neno NINA JAMBO LANGU limekufanya ujibu kwa jazba[emoji1787]
 
Kwa nilivyosimamia uchaguzi uliopita kulikua na form maalum unajaza na mawakala wanasign then unapiga ya rais tu kama mkoa tofauti,ya rais na mbunge kama Jimbo ni moja,sijajua kama utaratibu huu umebadilika ndani ya miaka mitano hii
 
Usiseme hivo...kuna namna nyingi za kushiriki mchakato mzima wa uchaguzi mbali na kupiga kura mkuu.
Kama kuna namna nyingi za kushiriki zitafute ujihakikishie mapemaaaa
Vinginevyo bado una siku21 za kuweka mipango yako sawa ukapige kura ulikojiandikishia
 
Mfano mimi kitambulisho changu nilipewa nikiwa eneo lingine lakini hilo eneo nikahama nikahamia sehemu nyingine na sehemu niliyohamia nikaenda kuandika jina kwenye daftari la wapiga kura.

Je siku ya kupiga kura nitaruhusiwa au sitoweza kupiga kura kutokana na kitambulisho kutokuendana na eneo husika?

Naomba ufafanuzi wadau.
 
Kama upo sehemu ulipojiandikisha utapiga kura ht kama kitambulisho sio cha eneo hilo, cha msingi n jina lako kuwepo eneo tukio ambalo utapiga kura
 

Uliendaje kuandika jina bila kupewa kitambulisho kipya mkuu??

Kwenye hayo maboresho ukibadili taarifa walikua wanatoa Voter’s ID card mpya nadhani
 
swali dogo maelezo kibao hata yasiyo na tija, itoshe tu kusema wewe ni miongoni mwa matabulalasa
 
Kwa maelezo yako maana yake ni kuwa umeshafanya marekebisho ya kuhama kwa hiyo utaruhusiwa kupiga kura.

Ni muhimu kufatilia kabla ili ujiridhishe kuwa utapigia kituo gani pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…