Kuna utaratibu wa kufuata ukitaka kuanzisha App Tanzania?

Hakuna "developer bora mmoja" kwa kila mradi.
Badala yake angalia:
1. Portfolio
Mwombe akuonyeshe:
Apps alizotengeneza
Zilizopo Play Store
Zilizopo App Store
Kama hana chochote cha kuonyesha, kuwa makini.


2. Anaelewa biashara au coding tu?
Developer mzuri:
Anaelewa biashara
User experience
Marketing
Scalability
Siyo coding pekee.


3. Ownership ya Source Code
Mkataba uwe wazi kwamba:
Source code ni mali ya mteja.
Database ni mali ya mteja.
Domain ni mali ya mteja.
Play Store account ni mali ya mteja.
Hili ni muhimu sana.


4. Documentation
Mwombe:
Technical documentation
Database schema
API documentation
Usikubali mfumo ambao developer pekee ndiye anaujua.
 
Vipi Kuhusu Kuibiwa Wazo?

Ukweli ni kwamba:
Wazo pekee lina thamani ndogo kuliko utekelezaji.
Kila siku developers husikia mamia ya mawazo.
Kinachofanya biashara ifanikiwe ni:
Execution
Marketing
Team
Mtaji
Wateja

Hata hivyo unaweza kujilinda kwa:
NDA (Non-Disclosure Agreement)
Mkataba wa kutofichua siri.
Development Agreement
Mkataba unaosema:
Nani anamiliki mfumo
Nani anamiliki source code
Ratiba ya malipo
Muda wa kukamilisha kazi
Matengenezo
Trademark
Baadaye unaweza kusajili brand yako kupitia Business Registrations and Licensing Agency.

Da'Vinci vinci
 
Bro umeupiga mwingi sana. Shukrani ngoja nitakurudia
 
Hiki tayari nishaandaa
 
I mean documents before meeting a developer
I understand , Do you have a prototype?

Prototype ni toleo la majaribio la app ambalo halijakamilika, lakini linaonyesha muonekano na jinsi itakavyotumika.
Mfano wa App
Kama unataka kutengeneza app ya POS/INVENTORY MANAGEMENT
Prototype inaweza kuwa na:

Login page tu
Dashboard ya mfano
Buttons zinazofanya “mock action” (hazihifadhi data halisi)
Screens chache tu
Lakini:

Haijakamilika
Haijawa na backend kamili
Mara nyingi ni ya kuonyesha idea tu


Aina za Prototype

1. Paper Prototype
Michoro kwenye karatasi
Inatumika kubaini design mapema

2. Digital Prototype
Inatengenezwa kwa tools kama Figma, Adobe XD
Inaonekana kama app halisi lakini haifanyi kazi kikamilifu

3. Functional Prototype (MVP)
Ina baadhi ya features halisi
Inaweza kujaribiwa na watumiaji


Kwanini Prototype ni Muhimu?

Kuonyesha wazo kwa wawekezaji
Kupata feedback mapema
Kupunguza gharama za kubadili mfumo baadaye
Kuepuka kujenga app isiyohitajika na watu
 
Sina prototype kiongozi
 
Sema hawa madeveloper wazawa huwa wanataja bei kama wamelewa, jiandae kisaikolojia unaweza lipa hela nyingi ukapata kitu cha hovyo!

Kuhusu kuibiwa wazo ni uoga wako tu, kila unachowaza kufanya watu walishafanya tayari!
Kama ulikuwepo kiongozi. 7.5M ndo wamechaji....
Noma sana
 
Ahaa kwa hiyo kufungua app na kuiweka playstore haiwezekani bila kodi za serikali au?
 
Achana kusajili wal kijisajili kokote uhalisia ni huu
Kama ni app Anza na Android Sheria za sasa kupublish app ni ngumu kuiko zile za zamani mfano google play Kuna aina mbili za account za developer Kuna personal na business/organization Kwa personal unataiwa kuwa na either nida, leseni ya udeleva au passport na account ya bank inayotumika na inayofanua transaction online sio virtual card aka prepaid kadi hapo unatakiwa kuaandaa ban statement ya hiyo account mfano nmb crdb n.k


Sha utatumia taarifa hizo kusajili personal account lazima utumie physical identify kama nilizotaja sio kopi au snap, Kwa personal account unatumia email utakaychaguanisha utalipia na ku upload hivyo viambatanishinkama bank statement, nida au leseni ya udereva au passport Kisha google wataverify taarifa zako na kukuruhusu ku upload app katika fomart ya AAB uki upload lazima utafute watu w kutest APp wanaitwa tester kwa siku 14 wanatakiwa kuwa active kutest app akileft Mmoja umefel test app Yako haipiti popote na ni at least 12 tester.


Hiyo ndio personal account Kwa sasa.

Organization haitaj tester ni faster kupublish app lakini lazima uwe na kampuni au taasisi hivyo una viambatanishinkama Tin, brela etc vyote vihusuvyo kampuni aka vitambuishi vya kampuni.

Kinachobaki ni wewe kutafuta wateja wako wa kutumia appp


Kwa apple store si haba kama unaanza pesa yao ni kama 200k Kwa mwaka tofauti na google 67k +++ onetime.

Nimechoka kuandika nadhani mambo mengine utajiongez au kutuipa kabisa ikibidi Anza naweb sababu wapo watakaokuwa wanauliza nataka web yenu si jui nini





nb natumia kishikwambi Cha mke wangu ni mwaimu so kigumu kuandika vizuri Iowa serious na Hela nigte dm nikutumie na wadau usiwafate kuuliza wafate kufanya kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…