kuna utata upatikanaji wajumbe mabaraza ya katiba

kuna utata upatikanaji wajumbe mabaraza ya katiba

iringa

Member
Joined
Feb 5, 2012
Posts
66
Reaction score
33
Kwa mujibu wa mwongozo uliotolewa na tume ya mabadiliko ya katiba, mabaraza ya wilaya ngazi ya mamlaka ya serikali za mitaa wajumbe wake watachaguliwa na wananchi kila Mtaa/Kijiji kisha majina yao yatapelekwa kwenye kamati ya maendeleo ya kata ambako nako majina yatapigiwa kura kupata wajumbe watakao wasilishwa tume ya katiba kwa uteuzi rasmi.

Utata uko hapa kama ifuatavyo:

1.Kwenye kila Mtaa/Kijiji mwongozo unasema wananchi (Tanzania bara) watapiga kura kupata majina 4 (Dar 8) ya wananchi waliojiandikisha kuchaguliwa kuingia kwenye mabaraza ya katiba. Mwongozo hausemi kama wajumbe hao watatakiwa kujinadi kabla ya kupigiwa kura ili wananchi wapate nafasi ya kuwachuja na kuchagua wajumbe sahihi. Kama wakichaguliw kwa kuangalia horodha ya waliojiandikisha kuna hatari ya kura kupigwa kwa mtazamo wa kujuana bila kupima uwezo wa mjumbe kwenye zoezi zima la mchakato wa kikatiba ambalo linaitaji uelewa mkubwa wa mambo .

2. Kamati ya maendeleo ya kata itachagua majina 4 (Dar 8) kati ya mengi yaliyopendekezwa kutoka kwenye Mitaa/Vijiji kupata wajumbe wa Kata kabla ya kupelekwa kwa mkurugenzi kisha tume kwa uteuzi. Je ni utaratibu gani wa upigaji kura utakaotumika? Kwa kuzingatia wajumbe wa kamati ya maendeleo ni wachache ukilinganisha na idadi ya wale wanaopigiwa kura.

kwani kila mjumbe akiwa na kura 1 kuna baadhi ya wagombea hawatapigiwa kura kabisa ama kuna uwezekano wa kila mjumbe kumpigia mgombea 1 tofauti na mwingine hivyo kukosa washindi. Je hilo likitokea busara gani itatumika? Kuna uwezakano tena wa wajumbe kupiga kura kwa kujuana ama kupenda jina la mtu kwani kuna uwezekano mkubwa tu wa wagombea kutofahamika kwa wajumbe.

Kwa hapa kuna hatari ya kupata wajumbe wasiostahili kama wagombea hawatapata fursa ya kujinadi mbele ya wajumbe.
Tujadiliane wana JF ili tupate wajumbe sahihi wenye sifa stahiki kama mwongozo unavyo elekeza.
 
Hiyo ni kweli! Tuelimishane kwani ata mimi nimetuma maombi ila sijui utaratibu utakuwaje?
 
Inaonekana hao wajumbe tayari wametayarishwa ndio mana wanataka wapatikane kwanza kabla ya kujua maudhui ya rasimu ya katiba. mimi nafikiri rasimu ya katiba ingetangulia ili tujue kilichomo na ndipo tujue aina na sifa za wajumbe wa kuijadili.Kwa sifa za sasa zinazotajwa tayari inaonekana rasimu yenyewe haiko serious na hivyo haiitaji watu waelewa bali inahitaji akidi tu ili kukidhi matakwa ya sheria iliyounda tume. usanii mtupu.
 
Back
Top Bottom