Kuna utekaji na mauwaji Kisemvule Pwani, nani anajali?

Kuna utekaji na mauwaji Kisemvule Pwani, nani anajali?

chala41

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2024
Posts
300
Reaction score
606
Jana usiku wakati naongea na moja ya ndugu zangu anaishi kisemvule kwa pembe au wanaita kisemvule mpera.

Tumeongea mengi pamoja na salamu za hapa na pale akanisimulia kuwa huku baba hali imebadilika sana kuna hali ya sitofahamu watu tunaishi kwa mashaka sana na watoto zenu.

Kwa sababu hivi karibuni kuna baadhi ya watoto walikuwa wanapotea katika mazingira ya kutatanisha na kuokotwa wakiwa wamekufa na tayar ikiwa wametolewa viungo kama Figo na moyo pamoja na sehemu za siri.

Aiseee sikuamini hii cenario lakin ni vitu ambavyo vinatokea katika dunia ya sasa na hizi zote ni dalili za ushirikina tu hakuna kingine zaidi

Akazidi kuenda mbali zaidi na kupeleka law ama kwa wanasiasa na serikali kwa ujumla ya kuwa kwa nini uchaguzi ukifika vitendo kama hivi viovu vinashamiri sana sana. Na hakuna mtu anaeshikwa na hata Doria tu za kawaida kuona kama serikali imeguswa na hili suala pia hakuna.

Kama watanzania tumepoteza utu sana mpaka kufikia mtu kutoa roho ya kiumbe kwa maslahi madogo sana
 
IMG-20240714-WA0689.jpg
 
Huenda haya ndio Yale Rais amesema na kukukea akiwa na machifu kwamba Watanzania waambiwe kwamba Cheo hakipatikani Kwa kutumia mambo hayo.
 
Hizi issues Wala sio drama. Ni hivi mambo ya kuwatoa watu Figo na sehemu zingne za mwili yalikua kwa Kasi sana China, S. Korea na India.

Sasa Tanzania pia imeanza upandikizaji wa Figo n.k kwahiyo mtu ambaye Yuko kwenye hayo mambo akikuona anaona Pesa tu kwenye viungo vyako vya mwili.

Kama nchi inatakiwa kua na Sheria thabiti ya upandikizaji viungo kama ulaya na marekani. India na china mtu anaeza kutekwa tu na wakamtoa hivyo viungo. Kueni makin
#No malice to anybody
 
Hizi issues Wala sio drama. Ni hivi mambo ya kuwatoa watu Figo na sehemu zingne za mwili yalikua kwa Kasi sana China, S. Korea na India. Sasa Tanzania pia imeanza upandikizaji wa Figo...

Mzee baba unafiri figo na internal organs zinapandikizwa kizembe tu hivyo?
 
Yaan huyo mtekaji ndo tumkamate mtaani kwetu nadhani atakua mfano yaan mateso tutamayo mpa hata shetani atakuja kujifunza maana hawa wapuuzi wabakatisha ndoto za vijana wetu kwa tamaa za pesa.
 
Back
Top Bottom