Immortal Joe
New Member
- Nov 10, 2021
- 3
- 1
Ni wakati ambao mabadiliko ya tabia ya nchi yamechukua nafasi katika ulimwengu huku tukiwa tunashuhudia ongezeko la joto na upungufu wa mvua katika baadhi ya maeneo nchini. Mazingira yanatuma taarifa kwa ulimwengu kama tunahitaji kuyategemea basi tunajukumu la kuyatunza na kuyalinda.
Viongozi wa Mataifa(makubwa kwa madogo) bado wanaendelea na mijadala ya kutafuta utatuzi juu ya mabadiliko ya tabia ya nchi ni jambo la kupongezwa kuona Mataifa yakiondoa tofauti zao na kukaa meza moja ili kuja na mkakati mzuri ambao utawezesha kupunguza au kuondoa kabisa makali ya athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.
Mabadiliko ya tabia ya nchi yashatokea na athari zake zinaonekana swali ni Je sisi kama taifa wananchi na serikali tumejiandaaje kukabiliana na hizo changamoto ambazo ni matokeo ya mabadiliko ya tabia ya nchi?
Mosi tuna chakula cha kutosha endapo kwa bahati mbaya kutatokea balaa la njaa? Na ni kwa muda gani tutaweza kuishi na balaa la njaa bila ya madhara makubwa haswa kwa raia wa daraja la chini?
Pili ni mikakati gani tuliyonayo kama taifa kudhibiti uharibifu wa mazingira?
Tatu ni kuwa kilimo cha kisasa na umwagiliaji ndio mkombozi pekee wa kutuepusha na uhaba wa chakula na kwa bahati nzuri tumebarikiwa kuwa na vyanzo vingi vya maji kuanzia maziwa, mito na mabwawa je tumejiandaaje kushiriki na kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji?
Kila mwananchi kwa nafasi yake atunze na kulinda mazingira ili kuwezesha dunia kuwa mahali salama kwa kuishi.