Kuna uwezekano wa Taifa Stars kusonga mbele?

Algeria tutawashinda. Hawatatufunga hata mechi moja. Kwa Stars ndio mwisho wao. Mkwasa ndiye mwisho wa manung'uniko yetu. Stars tunawaamini

Mkuu midfielder ni tatizo sana katika nchi hii.Wachezaji wote wangecheza mpira wa kujituma kama kanavaro wa yanga au Ulimwengu basi angalau tungesema chochote lakini si hii ikifunga 2 au 3 basi imeridhika na kuona imesonga mbele...Naipenda sana Taifa stars lakini nilichokiona Malawi kwa dakika chache za mwisho nilizoangalia mpira sikuamini na kocha aliniacha katika mshangao mkubwa sana kwa kuweka Boko wakati viungo vilikufa kabisa.Tukipita hapo nitafurahi zaidi mkuu
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa Stars iliyoteuliwa hivi karibuni na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Bwana Farough Baghozah leo hii amekutana na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam na kuitambulisha rasmi kamati hiyo.


Katika kamati hiyo ya Taifa ya Stars wapo Michael Wambura – Makamu Mwenyekiti, Bi Teddy Mapunda – Katibu, Wakili Imani Madega – Mweka Hazina, na wajumbe wengine ni Juma Pinto, Isaac Chanji, Salum Abdalla na Moses Katabaro.


Pia Mwenyekiti amechukua fursa hiyo kutangaza kamati ndogondogo na wajumbe wake kama ifuatavyo:


1. Maandalizi ya timu, zikiwemo huduma kwa timu ya Taifa stars
Mwenyekiti – Imani Madega


Wajumbe – Msafiri Mgoyi,Teddy Mapunda.
2. Uhamasishaji wa mchezo (Michezo ijayo) na Masoko
Mwenyekiti – Juma Pinto


Wajumbe – Baraka Kizuguto, Mlamu Ng’ambi, Charles Hamka, Hashim Lundenga, Maulid Kitenge, Shaffih Dauda, Salehe Ally, Peter Simon, Edo Kumwembe na Mahmoud Zubeiry.


3. Kamati ya Fedha

Mwenyekiti – Farough Baghozah

Wajumbe – Teddy Mapunda, Michael Wambura, Imani Madega, Juma Pinto, Isaac Chanji, Moses Katabaro na Edgar Masoud.


4. Mikakati ya ushindi – itakuwa na kamati ndogondogo na zitakuwa na wajumbe mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti Farough Baghozah, Teddy Mapunda, Mohamed Nassoro, Philemon Ntahilaja, Isaac Kasanga, Cresencius Magori.

Pia kamati imetangaza kauli mbiu ya ushindi inayosema “NCHI YETU, TIMU YETU, TAIFA LETU, USHINDI WETU” itakayoanza kutumika kuanzia leo hii. Pia Kamati imemteua Bi Teddy Mapunda kuwa msemaji mkuu wa kamati hiyo.

Timu inatarajia kuweka kambi Nje ya Nchi kwa takribani siku 12 ili kujiandaa na mechi dhidi ya Algeria Novemba 14 Dar es salaam, na Novemba 17 nchini Algeria.


Aidha Mwenyekiti alitumia nafasi hiyo kuwaomba Watanzania wote warudishe imani kwa timu yao, wajitokeze kwa wingi kwenye mechi ijayo tarehe 14 November dhidi ya Algeria hapa nyumbani. Pia akatoa wito kwa Watanzania Wote kuchangia timu kwa hali na mali (Madawa, Maji, vifaa vya michezo na kadhalika)…aliongeza ‘Mwenyekiti wa Kamati Bwana Farough Baghouzah.
 


Mbwembwe za TFF hizo.
 
Kwenye Soka lolote laweza kutokea, muhimu ni kujijenga Kisaikolojia tu na kutoa woga wa kuogopa team pinzani,

BUT....

Algeria mziki wao sio wa kitoto,so inatakiwa maandalizi makubwa kwa Stars
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…