Kuna viashiria vya kijamii na kiuchumi kwamba huenda ndio mwisho wa utawala wa CCM

Kuna viashiria vya kijamii na kiuchumi kwamba huenda ndio mwisho wa utawala wa CCM

mwengeso

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2014
Posts
9,227
Reaction score
6,670
Kinachoendelea nchini kwa sasa, kisiasa, kuna viashiria vya kijamii na kiuchumi kwamba huenda ndio mwisho wa utawala wa CCM.

KIJAMII
Kuna matukio kadhaa makubwa ambayo yanamomonyoa misingi imara ya usalama wa kijamii. Matukio hayo, yanayotokana na uongozi wa CCM, ni kama vile wanasiasa wa upinzani:

[emoji830]︎ kunyanyaswa;
[emoji830]︎ kutekwa;
[emoji830]︎ kujeruiwa;
[emoji830]︎ kufunguliwa mashtaka, nk.

Matukio hayo yanathiri siyo tu viongozi hao wa siasa bali pia, na hasahasa, familia zao, ndugu na marafiki. Ikizingatiwa kuwa ni karne ya TEHAMA, matukio hayo siyo siri tena.

Kwa sababu hiyo kizazi kipya, kitakachopiga kura 2025, kinajenga chuki dhidi ya utawala uliopo.

KIUCHUMI
Miaka mitano ya utawala wa Awamu ya Tano, miradi mingi ya kimkakati, ujenzi na uboreshaji wa miundo mbinu ya usafiri na huduma za jamii (afya, elimu, maji) zilifanyika kwa pesa za ndani kutokana na kodi za wafanya biashara wakubwa ambao awali walikwepa kulipa.

Awamu iliyoko madarakani, pamoja na kuwabana wanyonge kwa tozo, misaada na mikopo ya nje, pia imewapunguzia kodi wawekezaji ili kuwavutia.

Mikakati hiyo ya kiuchumi, hakuna shaka inawaweka wanyonge, wengi wao vijana, katika hali ngumu. Isitoshe, jeshi hilo la vijana, liko kwenye sekta isiyo rasmi, ambayo kwa bahati mbaya au kwa makusudi, utawala ulioko madarakani, haujawatendea haki inayostahili. Mazingira yao ya kufanya biashara, na shughuli zingine za kiuchumi, siyo rafiki kama awamu iliyopita.

Je, ni viashiria vya mwisho wa utawala wa CCM?
 
Kiujumla CCM wamepotoka kutoka kwenye misingi, kutoka kwenye nguvu ya UMMA mpaka nguvu ya DOLA.

CCM imetoka kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi(wengi) kimekua chama cha mwenyekiti(Raisi), wabunge, mawaziri, matajiri na watu wachache wenye ushawishi lakini ukiangalia sasa CCM inatumia gharama kubwa kubaki relevant ie kugawa nguo bure,kununua wanachama na kuzuia shughuli za kisiasa kwa vyama vingine lakini wao wanafanya kwa mgongo wa kusimamia ilani
 
Japo unapigania tumbo lako ili angalau uweze kujaza choo chako, lkn ki ukweli umeandika ujinga zaidi ya ujinga wenyewe.
 
Kila chenye mwanzo haikosi mwisho ila sababu ulizotoa hapo hazina mashiko kabisa,

Hizo sabab za kijamii zimetokea toka utawala wa nyerere na bado ccm ipo madarakan mbk hii leo.

Pia vijana wengi sio wapiga kura hususani wa chadema hawana hata vitambulisho vya kura,

Nakumbuka mwaka 2015 - 2020 kusini vijana tulikua tunajazana kweny mikutano ya chadema lakini siku ya kupiga kura wote tulikua vijiweni kupiga soga.
 
Back
Top Bottom