Kuna vimaneno nikikuona unavitumia basi moja kwa moja nakuweka kwenye kundi baya

Shida na raha

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2014
Posts
3,773
Reaction score
3,471
Habari za kuamka wakuu.

Kuna vimaneno ambavyo vinaibuka mitaani ambavyo hata huwezi chanzo chake vimetokea wapi.
Hata hata hivyo, mimi nikikusikia unayatumia moja kwa moja nakuweka kwenye kwenye kundi ambalo nalifikiria na moja ya makundi hayo hautakaa usiwe na kundi moja wapo.

Kuna haya maneno kwamfano "Vele, wooooza, mwana" na mengineyo ambayo nimeyasahau. Yaani nikikusikia hata kama wewe ni rafiki yangu basi naanza kujitenga na wewe aidha utakua unavuta bangi, unakunywa mapombe kupitiliza au madawa ya kulevya.

Na sisemi hivi kwasababu siyatumii mimi hapana, nimejaribu kufanya uchunguzi nikagundua yanatumiwa na watu hao na humu wamo akina shem wangu Shunie anatumia.
Na pia kama kuna mtu anabishana na mimi kwa hili nnalosema afanye uchunguzi na yeye atapata majibu kama nasema uongo au ni ukweli.
Nawakilisha.
 
Oyaaa, vele, woooza veepe mwanaaaa, upo poa wangu?
 
Wooozaaa kamanda long time mwana upoo mambo mengine vepeeeeee
 
Ukinitumia message eti "mmbo wng, thnx, y" sikujibu na utasubiri sana.
 
Kwa hiyo Shunie atakuwa mlevi.... mhuni (mdangaji) na mvuta bangi kabisaa.....

Aiseee......
Huyu mtoa mada tu hajui maneno mengine yanavyotumika ndo shida yake. Aseme ni wapi alisikia mvuta bangi au mla madawa ya kulevya akisema wooozaaa. Kwanza ni neno la kike ye mwanaume hawezi elewa misemo ya watoto wa kike ndo maana kakazania ni neno baya. Tutalitumia kama kawa kama dawa asolipenda atajimurder
 
Kuna mwanaume mmoja Jana kanitext .. Kaniita my .. ***** ... Kilichomkuta atawasimulia hadi wajukuu zake .. Watu wengine wajinga sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…