Kwanza niwakumbushe wanaJF wenzangu kwamba mustakbali wa nchi hii upo mikononi mwetu wenyewe, wala hakuna mgeni atakayefikiri na kufanya maamuzi kwa niaba yetu-kwa manufaa yetu. Sote tunafahamu ni kwa kiasi gani swala la lugha linalikanganya taifa letu ktk midani ya utoaji elimu kwa ufanisi na kuongeza uelewa wa wananchi kwenye stadi mbalimbali za maisha. Mipango yetu ya elimu imekuwa na dosari nyingi tunazopaswa kuzirekebisha, mtiririko wa lugha ya kufundishia umekuwa ni kikwazo na madhara yake tunayajua na ni dhahiri.
Elimu ni kufundishana maarifa - yaani yule anayeelewa (mwalimu) aambukize maarifa yake kwa wale wasioelewa (wanafunzi), kwa kutumia Lugha. Kati ya mwalimu na mwanafunzi daraja ni LUGHA- wala hakuna mbadala, na kubabaisha katika lugha ni sawa na kuwa na barabara nzuri na pana kila upande ilhali daraja la kati ni jembamba na dhaifu - tusitaraji tija, hata kwa kudra. Kiwango cha elimu kitazidi kushuka na asilimia kubwa ya wasomi wetu wataendele kuplay second fiddle kwenye soko la ajira la ndani na nje.
Hapa sina kusudi la kuanzisha mjadala wa lugha gani itumike kufundishia, la hasha... lengo langu ni kuanzisha hoja ya "NINI KIANZE KATI YA WANANCHI KUWA NA MWAMKO WA KUPENDA KUSOMA VITABU, AU WACHAPISHAJI NA SERIKALI KUWA NA MWAMKO WA KUCHAPA VITABU VINGI KWA LUGHA INAYOELEWEKA NA WENGI.
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na tafiti kadhaa zinazoonyesha kuwa kiwango cha elimu kinaporomoka kwa sababu mbalimbali lakini mojawapo ni ya jamii yetu kutokuwa na utamaduni wa kupenda kujisomea... hiyo ni sahihi... lakini ni kwa nini hatupendi kujisomea? Kwangu mimi jibu ni moja na la wazi kabisa; watanzania tulio wengi tunapita maisha yetu yote ya utotoni tukiwa tunaelewa lugha ya kiswahili tu, na kwa wale wachache wanaofanikiwa kujifunza na kuelewa lugha ya kiingereza wawapo secondary na vyuoni bado uelewa huwa ni wakutosheleza matumizi ya kumeza na kutema tu...
Kwa hali hiyo, iwapo kweli kujisomea ni muhimu ili kupata kizazi cha wasomi wa kweli na mambumbumbu wenye shahada na stashahada za kutenda, ni vema sasa watunga sera wageuke na kuangalia uhalisia badala ya kuinyooshea kidole jamii kwa kutopenda kusoma vitabu ambavyo kwa kweli ni kama havipo!..
Tembelea maktaba au duka lolote la vitabu, ondoa vitabu vile vya kiada ambavyo hutumika kufundishia, halafu angalia utabakiwa na vitabu vingapi vya kiswahili, kisha ni vingapi vya kiingereza na lugha nyingine za kigeni. Ukishapata jibu jaribu kupiga hodi kwenye ofisi kuu ya takwimu, waulize waheshimiwa eti kuna watanzania wangapi wanajua kusoma vizuri kiswahili, na wangapi kiingereza!... Lazima tujue kuwa kwa sasa hatuhitaji watu wasome tu... ni lazima WASOME NA WAELEWE... kwetu sisi watanzania kiingereza ni muhimu, ila kiswahili ni muhimu zaidi...
Halafu ukitaka kujua ni kwa nini vitabu vya kiswahili ni vichache kiasi hicho, usiulize, nenda kwa mtunzi yeyote (Mimi ni mmojawapo), muulize kama ana muswada wa kitabu alioundika akashindwa kuuchapisha, mwombe uende naye kwa wachapishaji(publishers)... akikubali jibu utalipata huko na muswada utarudi tena kabatini...
Sisemi kwamba miswada yote inastahili kuchapishwa, ila hakuna mantiki ya mapublisher kukataa miswada ya vitabu vya kiswahili ambavyo watunzi wanatumia muda na rasilimali zao kuiandaa, huku wakiwa hawana miswada iliyo bora kuliko hiyo... Wanakumbuka tu kuwa wao wanahitaji faida na wanasahau kabisa kuwa jamii inahitaji maandiko hayo kwa wingi sana, hasa kipindi hiki... please think twice b4 u turn u r back on our scripts!
To cut a long story short, nawauliza ndugu zangu wa BAKITA na BODI YA HUDUMA ZA MAKTABA; hivi kwa takwimu walizonazo sasa, tuna vitabu vingapi nchini vilivyoandikwa au kutafsiriwa kwa lugha ya kiswahili? na je vinawianaje na idadi yetu? na je miongo kadhaa ijayo idadi yetu itakapoongezeka ipo mipango ya kuhakikisha vitabu vya kiswahili navyo vitaongezeka?..
Ni mtazamo tu.......... masela msi...................