Kuna wa kumzidi Rose Muhando?

Rexwinton

Member
Joined
Mar 26, 2021
Posts
74
Reaction score
137
Hivi kuna muimbaji wa muziki wa injili aliwahi tokea kumzidi Rose Muhando, naongelea wote wakike na wakiume?

Kwangu mimi bado sijaona! Ukianza na Uwe Macho, Nibebe, Utamu wa Yesu, hizi album zilikuwa ni mwisho wa matatizo aisee!

 
Wako tele kama vile

Martha mwaipaj
Christophe
Bonny mw
 
Unaimba nje ya mafundisho sahihi ya biblia...kwa hiyo hana lolote
 
Tatizo mnaskiza gospel kama burudani ila ukitaka gospel kama injili ya kweli na ibada msikilize upendo kilahiro na upendo nkone
 
Yuko vizuri mno kwenye nyimbo za injili wa aina yake peke yake
 
Reactions: THT
Akina Mondi wenyewe hawaoni ndani . Ngoma zake hadi bar zinagongeka safi. Energy kubwa kwenye nyimbo zake imefanya zinoge. Bahati mbaya alipoteana
 
Rose Muhando kwakweli Ni GOAT kwenye gospel, Kuna watu Mungu anawapa karama jamani na huyu mama alikua mmojawapo, Mungu aliweka kitu kikubwa Sana kwa Rose ile album yake ya kwanza ilitoka nikiwa mdogo Sana nakumbuka baba alinunua nilikua siruki nyimbo hata moja yaani nyimbo zote zinasikilizika na kugusa mpaka Sasa hivi nimekua mtu mzima ile album bado Ina ladha ileile and more meaningful Sasa hivi nikiisikiliza kwa sikio la kiutu uzima,dah Rose kwakweli Basi tu.anakuambia " naonaaa Kama maonoo kumbe ndivyo ulivyo, nilidhani Kama ndoto, kumbe ndivyo ulivyo babaaa"
Kuna ule anakuambia. " Sisi tuna ujasiri mwingi hatumo, hatumoo ,hatumo miongoni mwao wenye mashaka hatumo".
Kwa kila majira Kuna kusudi na Rose kwa majira yake alilishi kusudi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…