hata mimi
JF-Expert Member
- Oct 17, 2017
- 1,356
- 1,442
Habari,
Nimezoea kuona wahudumu wakichukiwa sana wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao ya kila siku katika zahanati vituo vya afya na hospitali mbalimbali hapa nchini
Nitatoa mifano hapa
A. Wakati wa kuona wagonjwa muda ukiisha mnafukuzwa na kwa wale vichwa ngumu ndo wanafukuzwa kama paka mwizi
B. Muda wa kufanya usafi (mara nyingi kabla ya saa 2 asubuhi- kabla ya muda wa kazi) hapo mtaambiwa mtoke nje wote wabaki wale wagonjwa wasiojiweza kabisa wodini. Hapo manesi wenye zamu watafanya shughuli zote za usafi tena usafi wa nguvu
C. Mgonjwa anapo admittiwa au akiruhusiwa maswala yote ya kitanda neti na matandiko yake ni juu ya nesi
D. Kila kitu mtafanya kwa maelekezo ya nesi mfano kutangaziwa kila ikifika muda wa kumpa mgonjwa dawa, muda wa kushusha na kuchomoa au kukunja neti, muda wa kufungua au kufunga madirisha/vioo muda wa kulala au kuamka
E. Ukifika mapokezi tu hatua za kufuata kuingia sehemu nyingine zote utazijua kwani kila utakapofika anakwambia chukua hiki nenda nacho chumba namba fulani upande fulani au mlango/dirisha fulani
Sasa kuna kuna baadhi ya vituo vya huduma za afya nimeshangaa kuona mambo ni tofauti yani mpaka nikajikuta naboreka
Mfano
1. Watu wanaingia muda wowote kuona wagonjwa na hata wakikutwa watafukuzwa tu pale ndani lakini wakiwa nje ya wodi pale wanaangaliwa tu na wanapiga kelele katika vigenge vya stori mara nyingine mpaka mlangoni
2. Wenye wagonjwa wao ndo wanaoamriwa kufanya usafi wodini na mazingira ya nje pale wodini
3. Ukiruhusiwa basi ruhusa yako itakamilika baada ya wewe kufua matandiko (mashuka) yote waliyokupatia watoa huduma
4. Kama ni mgeni eneo hilo utakoma maana huelekezwi wala nini na ukiuliza unaonekana msumbufu. Mtu anakupa tu kama ni daftari au cheti au kikaratasi bila maelezo yoyote au anakwambia nenda maabara, kwa daktari, dirishani au sehemu fulani ukimwambia sijakuelewa hebu nielekeze tayari ugomvi
5. Mtu anaeleza namna anavyojisikia daktari anaandika tu kisha anakwambia nenda maabara (kisha) au nenda dirisha la dawa bila maelezo yoyote walla ABCs juu ya kinachokusumbua. Haya sasa hilo tuseme anaona haina haja maana watu ni wengi labda au kwakuwa mtu hajauliza pengine lakini sasa iweje hata mimi ninayeuliza nionekane msumbufu tena unakuta hakuna hata msururu?
Kingine hapohapo ni juu ya mwenendo au mlolongo ule wa MAPOKEZI[emoji654] DAKTARI[emoji654] MAABARA(baada ya malipo) [emoji654]DAKTARI[emoji654] DIRISHA LA DAWA(baada ya malipo)
naona kwingine kuna baadhi ya hatua humo wanakamata wao lile faili ili kuepuka mambo fulani fulani lakini kwingine hatua zote unapitia huku umepewa daftari lako ushike mwenyewe
6. Hakuna maelekezo yoyote juu ya dawa, malazi wala taratibu nyingine za pale wodini. Nakumbuka niliumwa nikalazwa sehemu fulani aisee kila kitu ni mpaka tuulize wenyewe lakini ukisubiri kupewa maelekezo imekula kwako
Mfano dawa imeandikwa kwenye daftari (file) ambalo analo nesi mwenyewe lakini unapewa unywe bila kuambiwa unakunywaje, kulala wauguzi wetu walikuwa hawalali vya maana ni kelele za stori tu mpaka karibu na asubuhi
Madirisha mnajiamulia kufunga au kufungua muda wowote, neti wengine wanapuuza/wanasahau kushusha kabisa au wengine inafika mpaka asubuhi daktari anaingia mtu yupo ndani ya neti
Hayo na mengine mengi tu nimeona sehemu mbalimbali na si kwamba yote mabaya bali mengine yamebuniwa kwa namna nzuri tu ila kuna changamoto ambazo zimeachwa bila kuzishughulikia ndo zinaleta madhara
Kwa mfano
1. Kwenye kufua mashuka nimeona hakuna kukaguliwa wala kusimamiwa eti wakiamini watu wazima hawana haja ya kufanyiwa hivyo. Matokeo yake watu wanaloweka mashuka kwenye maji (sijui tuite kuchovya) na kuyaanika kisa yeye anakwenda zake nyumbani na mgonjwa wake wanaobaki/watakaokuja watajua wenyewe
2. Usafi wa maeneo hayo kama tujuavyo kunahitaji umakini mkubwa sana lakini watu hao hawapewi kifaa chochote kile wanashika kila kitu kwa mikono yao, kifaa wanachotumia sanasana ni fagio tu
3. Watu wasipopangiwa muda wa kulala (siyo kusinzia maana najua haiwezekani) basi wanasumbua wagonjwa kwa kelele usiku pia wanajisahau katika uhudumiaji unakuta muda mgonjwa anataka kwenda haja muuguzi wake yupo bize na stori au ndo kwanza anasinzia ile asubuhi sasa ni nani atamkunjia/atamfungulia neti atoke
4. Kutandika kitanda na kuweka neti wengine hawana uwezo huo kivile lakini unakuta nesi anamkabidhi muuguzi vitu hivyo afanye mwenyewe mara tu baada ya kufika wodini na mgonjwa aliyeadmittiwa kwa mara ya kwanza. Hapo mgonjwa anaweza kuwa katika risk zaidi kiafya siku ya kwanza tu mara baada ya kufika sehemu inayodhaniwa ni salama kwake kiafya
5. Uholela katika kufunga au kufungua madirisha nao una madhara yake kwasababu unakuta mnajaza mbu ndani au muda ambao mtu anahitaji joto mwingine joto limepanda anafungua dirisha apate kaupepo
6. Kutibu tu bila kuambatisha na maelezo mengine ya mdomo mtu huyo anaweza akawa anakuja hapo kutibiwa kila siku kwakuwa hajui anapokosea
7. Hatua zile za mlolongo wa upataji wa huduma zikifanywa kiholela zinaweza kuleta shida mfano pale kutoka maabara kwenda kwa dokta huku umepewa majibu yako mkononi, kwa mwenye kuelewa amenielewa.
Mfano mwingine ni zile hatua za kuambiwa malipo kwanza kabla ya huduma, pale manesi wengi wanajidai kurahisisha eti umalize mambo yote then ulipe mwishoni kinachotokea kwa kujumlisha na mfano uliotangulia nadhani utainyima mpaka serikali mapato.
Sikutaja mifano hapa ila ieleweke tu hicho nilichokieleza kipo na wahusika wabadilike pale inapobidi na pale pa kuboresha waboreshe. Hatahivyo, no one is perfect except god kwahiyo pale ambapo nimeandika pumba siyo lazima kupakomalia.
Asanteni