Daudi Kempu
Member
- Dec 6, 2024
- 26
- 56
Utofauti ni kuwa, wewe unaumia sasa hivi, mwenzako aliumia jana, mwingine aliumia juzi, na mwingine aliumia miaka mingi iliyopita.
Umewahi kujiuliza, kama hayo maumivu utaishi nayo miaka kumi zaidi, yatakuumba kuwa kiumbe cha aina gani?
Kila mtu ana zamani yake ambayo, kama ingewezekana angeifuta kwa kifutio cha moto; isahaulike kama haikuwako mwanzo.
Zamani ni kama tu makovu; mengi ni ngumu kufutika. Na kadri tunavyojitahidi kuyafuta, pasi na utulivu tunaambulia kutengeneza majeraha mapya.
Hakuna namna utaumia zaidi ya vile umeruhusu.
Nakubali, maumivu huja mahali yasipotarajiwa kabla ndo maana huutafuna sana moyo.
Kuvunjwa moyo, hutokea kwa watu tuliowaamini kuliko namna tunaweza elezea, ndo maana kuna muda tunahisi kukata tamaa.
Lakini, ni sawa vile tunavyojitendea'ga' baada ya kupitia uzoefu huo mchungu?
Ni sawa kukosa usingizi kwa miaka kadhaa na kujipalia sonona?
Ni sawa kushindwa kula na kujichumia madonda ya tumbo? Ni sawa kujipuuza na kujiachaniza kisa tu umeruhusu kupokea maumivu kuliko unavyomudu?.
Uonavyo wewe, unajitendea haki?
Kuna pahala ili usogee ni lazima ukubali ukweli na uchambue ya kubeba na ya kuacha. Kuna mizigo ni hatarishi kwa safari ya ndoto zako.
Kuna watu kuwabeba kunahakikisha anguko lako. Kuna maumivu kuishi nayo na kuyakumbatia ni kama kuishi na adui anayekuua taratibu.
Kama unaweza japo kidogo, jifunze kuipenda nafsi yako kiasi cha kufika wakati wa kusema, "enough is enough"
Hakuna mwanzo wa furaha wenye tija bila kuruhusu mwisho wa huzuni ufike. Futa machozi. Vuta pumzi ndefuu, kisha achia...tuliza akili, fanya maamuzi sahihi.
Wewe ni wa thamani kama utaendelea kuwa mtu salama kwako na kwa wanaokuzunguka. Uchungu na maumivu vinakufanya uwe adui kwako mwenyewe, na kwa wale unaowathamini.
Tuwajibike, tukubali kuna mahali tuliacha mlango wazi na mwizi akaingia na kuiiba furaha yetu.
Hatua ya mapema na ya makusudi ya kurejesha upendo binafsi inahitajika kufanyika ili kuokoa jahazi.
Kuna makovu yatatakiwa kuishi kama ushahidi ili mwisho tukubali; HATUWEZI KUBADILISHA KILA KITU.