Kuna wakati umri itakuwa kikwazo, cheza nao vizuri

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
Tukiweka kujifariji pembeni ukweli utabaki kuwa umri sio namba tu bali zinazungumza kitu na tena kwa kumaanisha hivyo sio vizuri kupuuza.

Ipo mifano ya wachache ambayo inatembea ikiwemo ya mmiliki wa KFC kufanikiwa akiwa mzee ila kwenye kumi yawezekana akawa mmoja.

Umri kuna muda unakuwa kikwazo kwenye milango mingi ya mafanikio mpaka ya kisayansi hivyo usibweteke ukiwa na matumaini kuwa kesho mambo ndio yatakuwa rahisi la hasha.

Kwenye maisha ya kazi tukiachana na majeshi kwingine ukomo ni miaka 45 na hata nje ya kuajiriwa bado nguvu zinapungua kadri umri unavyozidi na hatimaye kupunguza ufanisi wa utendaji kazi.

Kila hatua ya umri kuna mambo yanakuwa rahisi kufanyika ambapo ukivuka hapo utakutana na ugumu hivyo TUSILALE TUKAJISAHAU.

TUAMKE TUFANYE MAMBO KESHO ITAKUWA RAHISI KWA MAMBO YAKE NA LEO NI RAHISI KWA UMRI WAKE.
 
Sisi ni Nini? Wakati ni Nini? Hofu na mashaka ni Nini?
 
Wazee na wabibi wanaokaa Dar es salaam Huwa wanajiona wote ni vijana wa miaka 20.Maana Kila unapompa salamu ya heshima anaikataa anapenda asalimiwe bro mambo vip?kama vile Bado ni kijana mdogo.
Sometimes unaweza Kuta wewe umezeeka kabla ya umri Hadi unapomsalimia mzee anashangaa huyu si rika lake kabisa?
 
Utakuwa siyo mkazi wa Dar au wewe ndiyo wazee ambao mkipewa salamu na mtoto mdogo unaikataa Kwa kigezio Cha kujiona ni mdogo
 
71C98C79-285A-4A49-800F-E027A5508F8E.jpeg
Daslam ukishaanza kuitwa “Odo” anza kuweka mipango thabiti.

Uzee pia tunautamani Kwani kwasasa kuufikia imekuwa changamoto sana.
 
Back
Top Bottom