figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Mimi binafsi sijafurahishwa ni haya mambo ya kuendekeza ukoloni. sikatai watoto wetu kufundishwa kingereza, lakini hii ya kuwafundisha kuimba wimbo kwa kingerrza napingana nayo. unamfundisha wimbo wa taifa auimbe kwa lugha ya kigeni ili iweje? na kwa manufaa ya nani?. je huo wimbo utaimbwa wakati gani na wapi?. hivi kuna nchi tofauti na tanzania inayoweza kuruhusu watu wake waimbe wimbo wao wa taifa kwa lugha za kigeni.jirekebisheni bana. mia