kuna walimu wa Tanzania malimbukeni

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Mimi binafsi sijafurahishwa ni haya mambo ya kuendekeza ukoloni. sikatai watoto wetu kufundishwa kingereza, lakini hii ya kuwafundisha kuimba wimbo kwa kingerrza napingana nayo. unamfundisha wimbo wa taifa auimbe kwa lugha ya kigeni ili iweje? na kwa manufaa ya nani?. je huo wimbo utaimbwa wakati gani na wapi?. hivi kuna nchi tofauti na tanzania inayoweza kuruhusu watu wake waimbe wimbo wao wa taifa kwa lugha za kigeni.jirekebisheni bana. mia
 
Ndugu mzee wa Mia,usipende kugeneralize kosa la sehemu moja au mtu mmoja kua la wote kitendo cha wewe kusema walimu malimbukeni unatudhalilisha sisi walimu ingekua vema kama ungetoa mfano kwamba ulifanya utafiti kw a shule ngapi ukabaini hilo sasa sio vema kuwaita walimu malimbukeni wakati wewe hujafanya utafiti wa aina yoyote kwa mantiki hiyo tupeni utafiti uloufanya mpaka utuite malimbukeni,kushindwa kufanya hvyo ww ndio limbukeni kwa kuleta taarifa bila utafiti
 

Wapi huko tena kumbe we limbukeni
 
hzo shule zenu za mapesa mengi!hz z jk hta kithungu baadhi walimu ha2kijui. . . .
 
Mzee wa mia Atuombe radhi Walimu...na hii thread ifutwe

Hakika mkuu Zeticha akifanya hivyo atakua muungwana kwani kwenye jukwaa letu la Siasa kule namheshimu sana kwa hyo atuombe radhi
 
heading nimeiweka kiuwalimu zaidi."kuna walimu wa tanzania malimbukeni" na "walimu wa tanzania ni malimbukeni", hauoni tofauti?. au nikisema kuna ukimwi tanzania ntakua namaanisha watanzania wote wana ukimwi?. kama ndivyo samahani ndugu zangu, yatakuwa matumizi mabaya ya kiswahili changu.
Lakini hata hivyo ujumbe umefika ya kwamba sio vizuri kuwafundisha watoto wetu yale ambayo hatukufundishwa. wimbo wa taifa uimbwe kama ulivyo. ni hayo tu. Mia
 
mzee wa Mia tutake radhi. Hayo mambo yako kwenye Shule zenu za kibwanyenye huku st. JK A.k.a za kata hata kingereza tunafundisha kwa Kiswahili
 

kabisa mkuu huyu kijana yafaa apigwe bakora, ametudhalilisha.
 
Walikua wanaimba hivi??

God bless africa,bless all her leaders,wife and men and chidren eheh ndio hivyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…