Kuna wana JF wamepotea au wamebadili ID?

Dejane

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2014
Posts
50,587
Reaction score
71,492
Kuna hawa wanaJF walikua wana vituko sana, yaani kipindi cha nyuma kulizuka katabia ukitundika tu nyuzi utaona mtu anakuambia weka picha, hata saa zingine huo uzi hauhitaji picha utaombwa picha.

Nilikua nikicheka sana, maana wengine waligadhabika wakiona wameombwa picha, wengine nao wakaamua wawe wanaweka tu picha ili mradi kumridhisha, tangopori nadhani.

Yaani yeye alikua akitaka picha tu, wengine walimuambia we ukitaka picha nenda instagram picha kule zimejaa utaangalia mpaka utachoka hahaha, kulikua na vituko sana enzi hizo tunashukuru hako ka kero kalipotea nadhani [emoji23][emoji23]

Tusichukulie kila kitu serious bana maisha mafupi haya.
 
weka picha alikua anaipatia Tyta
ungetaka hata picha yako anakuletea

aliniacha hoi alipoleleta picha za pale temeke kwenye bidhaa pendwa maswali yalikua mengi kuliko majibu
Yaa Tyta alitusaidia sana kuweka picha ya kila kiaina
Hiyo picha yaaje mkuu??
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] weka picha
 
Wako busy na majukumu yamezidiii umri
 
weka picha alikua anaipatia Tyta
ungetaka hata picha yako anakuletea

aliniacha hoi alipoleleta picha za pale temeke kwenye bidhaa pendwa maswali yalikua mengi kuliko majibu
Aiseee nimeona nimebaki hoi kwa kuchekaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…