Kuna watanzania wako serious na kauli ya Rais ya viwanda

Kuna watanzania wako serious na kauli ya Rais ya viwanda

mzalendoalltz

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2015
Posts
828
Reaction score
709
Kuna hawa jamaa wanajiita WOP, Himo-Tuneries aisee wana Products za viatu, bags, football, mikanda, n.k vyoti ni ngozi original.

Niliwahi kununua kiatu miaka mitano iliyopita mpaka sasa utafikiri ni kipya na kwa sasa naona wanauza vitu vya kwa bei ya kawaida sana.Kwa kweli wananikosha Roho, sinunui tena bidhaa za mchina.

Mungu awabariki kwa kazi nzuri, tunaomba Serikali iwapunguzie baadhi ya kodi ili wazalishe kwa wingi na tupate nafuu sisi wananchi. Wananunua ngozi zetu wala hawaagizi kutoka nje, bali wanafanya wenyewe.
 
Promo sio
Mbona pale salasala huwa kontena za ngozi zinashuka
 
Woiso kajitaidi ila mwambie bosi wako Apache kuchukua reject material toka China anatuumiza wajasiriamari wadogo tunaonunua marighafi kwake, kwasababu mengi yanakuwa hayana ubora, mfano, vitambaa begi za mgongoni. Ni shiida
 
Leo nimenunua viatu vya ngozi toka la Ndugu Woiso. Ni vizuri, 100% leather kwa shilingi elfu 45. Nimekuwa nakosa viatu vizuri kwa bei inayoridhisha hapa kwetu. Nimekuwa nanunua nje kwa zaidi ya miaka 20. Ila kuanzia sasa nitanunua hapa kwetu tu.

Nawashukuru sana watu kama Woiso, na Rais anayeamini tunaweza.

Bado sijapata mafundi bora wa suruali na mashati. Kama wapo tusaidiane kuwatangaza.

It can be done, play your part.
 
Back
Top Bottom