Kuna hawa jamaa wanajiita WOP, Himo-Tuneries aisee wana Products za viatu, bags, football, mikanda, n.k vyoti ni ngozi original.
Niliwahi kununua kiatu miaka mitano iliyopita mpaka sasa utafikiri ni kipya na kwa sasa naona wanauza vitu vya kwa bei ya kawaida sana.Kwa kweli wananikosha Roho, sinunui tena bidhaa za mchina.
Mungu awabariki kwa kazi nzuri, tunaomba Serikali iwapunguzie baadhi ya kodi ili wazalishe kwa wingi na tupate nafuu sisi wananchi. Wananunua ngozi zetu wala hawaagizi kutoka nje, bali wanafanya wenyewe.