Siku ya jana wakati naperuzi jf niliona kuna mdau anauliza kama kuna bloggers hapa bongo wanapiga zaidi ya milioni, ni swali lililonikumbusha mbali sana.
2020 kuna rafiki yangu anaefanyia kazi benki aliwahi kuniambia kuna kazi inaitwa blogging na kuna vijana wadogo tu (early 20s) huwa wanalipwa dollars, wengi milioni 1 hadi milioni 3, wapo idadi wastani wanapiga 4 hadi 7, na wapo wachache wanaofumua 8 mpaka 20+, nilimbishia niliona labda ni chai tu.
Kuna dogo nilimuunganisha field hio benki ila jiji lingine, nikamuuliza hilo suala na yeye alikiri wapo vijana wanaokuja kukusanya maokoto ya dola, ilibidi tusuke mpango nishuhudie mwenyewe, aliambia niende tarehe 22 ndio tarehe zao za malipo kutoka google.
Sikuamini macho yangu, kuna vijana wadogo wanapaki ndinga zao wanaingia wanaenda lile dirisha la western union wanatoa mpaka milion 4 na upuuzi, wale wachache wanaopiga dola zaidi hawatolei dirishani wanaingiziwa moja kwa moja kwenye account zao kwa njia inaitwa wire transfer
Nilianza rasmi utaratibu wa kusaka connection niliungwa group, kumbe na humo kuna matapeli wengi sana, niliuziwa account ya google adsense laki 2, nalogin inaandika disabled, alieniuzia kiswahili kingi. laki 2 nyingine ya kusetiwa blog ipatikane hewani ambayo sikuweza kuitumia baada ya adsense kufungiwa
Nikaona nijipe kwanza uzoefu kwa kufatilia group, ndio nikaja gundua dola zinapigwa kwa njia nyeusi, blogs zao wala hazina ishu, kinachotakiwa ni watembeleaji tu, hapo ndio wanaanza kushea zile picha za *** kwenye magroup ya Facebook, chini huwa kuna link unaambiwa uminye uone video kamili, ukiminya unapelekwa blog zao tayari sytem za google zinahesabu kuna mtembeleaji, dola zinaingia !!
Hawa jamaa ni wasiri sana, kushare ideas ni mpaka mjuane, kwenye magroup ni kurinfishiana tu muda wakufunga hesabu za siku, na tena hapo bado kuna matapeli, ukienda kuomba ufundishwe unapigwa na kitu kizito
Wale wenye blogs nyingine halali ni ngumu sana kufikia huko, wanaovuta milioni ni wa kuhesabu, wanacheza kwenye laki 3 hadi 7.