Kuna watu hawanuki mdomo kama panya

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mwanzo nilikuwa sijijui ila kadri siku zilivyokuwa zinakwenda nikawa nashangaa kila nikiongea na mtu anageukia pembeni, wengine wananitenga, nikachunguza na kujiuliza ni kwanini mwishoe alitokea rafiki yangu akanieleza ukweli kwamba ninanuka sana mdomo ila aliogopa tu kuniambia.

Kuanzia hapo mambo yakaanza kuharibika... nikaanza kupoteza kujiamini, kukosa furaha na amani hatimae nikaenda hospitali kuonana na wataalam wa kinywa na meno( dentist) lakini haikusaidia chochote zaidi ya kupoteza pesa tu.
 
Asante kwa ushauri wako na Mwenyezi Mungu akubariki sana ndugu

[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Ndio ila vijiwe zivioni kwa kweli
 
Dawa ni kuvikata vile VIFUKO kwa operasheni maalumu. Sijui kama umewahi kufanya hilo!


Kuhusu hilo niwe mkweli sijawahi mkuu zaidi ya kuondoa zile stones
 
Pole sana ndugu, lakini hilo ni tatizo dogo sana, na unalikuza zaidi katika akili yako linazidi kukuvuruga kumbe ni katatizo kadogo sana.

Nikushauri uanze tiba ya asili ya kubadilisha kabisa mfumo wako wa chakula pamoja na usafi wa meno.

1. Upe mwili wako nafasi ya kujitibu kwa kuachana na vyakula vinavyozalisha sulphur au vinavyosababisha harufu kuzidi maradufu kama vile nyama nyekundu, mayai, vitunguu nk. Na badala yake ule matunda na mbogamboga tupu angalau kwa miezi mitatu. (Na pia kama ulikuwa unameza madawa yoyote achana nayo).

2. Usinywe kabisa soda na vinywaji vyovyote vya kiwandani au vilevi na badala yake kunywa maji mengi sana angalau lita nne kwa siku na hata zaidi ya hapo.

3. Usitumie dawa za meno zenye flouride, na ikiwezekana tumia baking soda kwa kusukutulia angalau mara tatu kwa siku au zaidi ya hapo kwa kila baada ya mlo.

4. Sugua ulimi mpaka kwenye koromeo kule ndani kabisa na kwenye kuta zote za tonsils, na pia sugua juu kwenye PAA la mdomo, pembezoni na mdomo na kuzunguka fizi zote.

5. Chukua uzi wa kushonea nguo ingiza katikati ya meno safisha meno yote mpaka kwenye magego, ingiza katikati kila mahali.

6. Koroga maji ya chumvi fanya kama unayabwia mdomoni na kuyasukutua kisha yateme na meza kidogo kila siku baada ya kusukutua.

7. MAJI, MATUNDA, MBOGA ZA MAJANII ongeza kwa wingi sana.

8. Sali na fanya maombi. Nguvu za giza zipo.

9. Kila siku asubuhi unapoamka chukua malimau mawili makubwa yabinye kwenye kikombe cha maji kunywa. Kila siku angalau kwa miezi miwili uone hali ikoje.

10. Mwisho, fanya zoezi la kisaikolojia kwa kupuuza maneno na fikra za watu. Jiamini na endelea kujitibu. Hakuna aliye mkamilifu.
 

Mchawi maji mengi tu
 
Dawa ni kuvikata vile VIFUKO kwa operasheni maalumu. Sijui kama umewahi kufanya hilo!


Kuhusu hilo niwe mkweli sijawahi mkuu zaidi ya kuondoa zile stones
Sio lazima kuvikata, maana huwa vinakatwa pale ambapo tu mawe yanaota kila mara.

Kama hauna tatizo la kutoka vile vimawe, basi haina haja.

Na wakati mwingine unaweza ukakuta hakuna vimawe lakini kuna MAAMBUKIZI kwenye VIFUKO VYA TONSILS.

Yale maambukizi yanasababishwa na fangas au bakteria, na yanafanya kuleta HARUFU MBAYA.

Fanya jaribio la kuingiza mswaki kwa upande wa mshikio, ingiza kwenye vifuko vya tonsils chokonoa taratibu halafu unuse uone kama kuna harufu ama la.
 
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Sawa nimekuelewa vizuri mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…