Kuna watu hawatahesabiwa kwenye Sensa

Kuna watu hawatahesabiwa kwenye Sensa

Boss la DP World

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
2,318
Reaction score
8,464
Mfano naanza safari toka Mwanza jioni, naendesha mpaka Morogoro, nalala kwenye gari, kesho yake (siku ya sensa) naendelea na safari nafika zangu Dar.

Wanao hesabu watahesabu watu waliolala eneo husika usiku wa kuamkia siku ya sensa tu, kwahiyo watakaolala kwenye magari hawata hesabiwa, watakao lala mashambani hawatahesabiwa, watakao kesha baharini wakivua samaki hawata hesabiwa nk.
 
Kuna namna ya kuongeza hesabu za hao wanakesha kwenye mabar
 
Niache kwenda kupata moja baridi moja moto kisa sensa Mimi huwa sipendi ujinga hasa kwenye kunywa pombe nyie mnao penda hesabu hilo zoezi ni lenu sio sisi wa bia tamu
 
Kuna wale malaya waliokodi gest!

Sensa ni timilifu xa 99.5 ya kujua watu kuliko ya kuhesabu vizaz na vifo na wanaohama na kuhamia
 
Senza haijwahi kupata idadi sahihi ya watu, wakimaliza wanafanya hesabu za makadirio ndo wanatoa majibu ya idadi ya watu.
 
Kawaida ni kwamba kila kiumbe atahesabiwa, labda uamue mwenyewe vinginevyo kwa makusudi….. ila huko sijui gesti sijui kwenye mabasi kote huko taarifa huchukuliwa kwa utaratibu maalumu.
 
Yote sawa,ila kwenye M60 na laki8 na elfu kadhaa,kupoteza/kuinua hizo elf kadhaa kimahesabu huwa siyo tatizo.
Mtoa mada inaonyesha hesab ulizofundishwa hauziishi.Hukumbuki yale maswali ya kadili namba hii ktk Maelf,makumi elf mamia elf au mamilion ya karib?
 
Kwani si huwa wanapita kila nyumba, wanauliza kuja watu wangapi wanaishi hapa.
Hata kama haupo ili mradi unaishi hapo utahesabiwa.
Wakimaliza wanabandika bango ukutani au mlangoni wanaondoka.
 
Kwani si huwa wanapita kila nyumba, wanauliza kuja watu wangapi wanaishi hapa.
Hata kama haupo ili mradi unaishi hapo utahesabiwa.
Wakimaliza wanabandika bango ukutani au mlangoni wanaondoka.
Sio wanaoishi hapa, ni watu 'waliolala' hapo siku ya kuamkia sensa.
 
Back
Top Bottom