Kuna watu hufa mara mbili

They say you die twice.

One time when you stop breathing and a second time, a bit later on, when somebody says your name for the last time.
 
mshana jr Nakumbuka ulishawahi kuleta mada karibu inafanana na hii ya maiti kubembelezwa.... saa nyingine unaweza kufunga vifongo vya shati ukashindwa kabisa yani vinapishana. Nilikuwa siamini, yaani ni kama bahati au ndiyo nilikuwa napelekwa kwenye mafunzo. Nilihudhuria msiba wa kijana mmoja nadhani alikuwa na miaka kama 22 hivi, tulikuwa tunamuaga hapa Dar ili akazikwe kwao Dodoma.

Taratibu zote zilipokamilika ikiwamo ibada kwisha ikabidi kutoa heshima za mwisho. Watu wakatoa heshima zao, baba yake mkubwa akawa anaenda kutoa heshima alikuwa wa mwishomwisho hivi, cha kushangaza maiti ikaanza kulia na kutoa makamasi kama mtu aliye hai..

. ikabidi ndugu waitane nami nikasogea karibu ijapokuwa sikuwa ndugu... wakaongelea jambo hilo...mama mmoja aliyekuwepo hapo nadhani ni mtu wa Mbeya aliwaambia wachukue nguo zake waziweke ndani ya jeneza mpaka Dodoma. Na kweli walifanya hivyo na maiti ikaacha kulia. Nilistajabu sana kwani sikuwahi kuona maishani mwangu.

 
Duh!si mchezo duniani kuna mambo jamani.Hii thread inafundisha jambo kubwa na mahususi sana,Ninakuomba mtoa mada uendelee kutujuza zaidi juu ya habari za Watu wanaokufa hii itatupa somo zuri kwa kuwa hii ni field inayomuhusu kila mmoja wetu,na haina sababu ya watu kuogopa.
 
Eeeeeh!!!,hii nayo ni kiboko aisee.Watu wa afya kwa ujumla wake mnaona vitu vingi kumbe.
 
SOCIOLOGISTTZ kuna wavivu wa kufikiri waliiponda sana ile post lakini hawajui kuwa haya mambo yapo live kabisa
 
mshana jr

mshana jr njia yaangu ya kutafutia mkate wa kila siku ni nyingine kabisa ila unaweza jua na kupata exprience kupitia kusoma na kuzungumza na watu mbalimbali, ngoja niseme kidogo yale niliyo pata kusoma na kusikia kutoka kwa wahusika wenyew tena wale waliokuwa ni wafanyakazi wa mochwari kwa

kipindi fulani ila kwa sasa hawafanyi kazi hiyo, na wameweza sema maana unaambiwa kama waendelea fanya kazi humo yale uyaonayo na kuyasikia yabaki siri yako hata unaebadilishana nae shifti usimjuze otherwise huwe umejipanga haswaaaa tena kisawa sawa, ngoja niweke pozi nije niyaweke vziuri ASAP
 
Last edited by a moderator:
kuna story niliwahi kuisikia juu ya mortuary technician mmoja miaka ya zamani kidogo pale mawenzi regional hospital moshi.
alikua akiingia kwenye wodi za wagonjwa na yasemekana akimwambia mtu utanifuata basi ilikua haichukui muda mtu huyo anafariki...
je jambo hili linawezekana au ni story za kahawa?
 

Mwaka 1999 tukiwa nchi fulani hapo bara Asia tukaitwa kuhudumu mahali, kazi yetu ilikuwa ni kumvisha vizuri marehemu tayari kwa heshima za mwisho aliyekufa kwa kupigwa risasi na majambazi na kuporwa pesa nyingi

Jamaa alikuwa maarufu na mwenye pesa hivyo ukumbi ulikuwa umefurika watu wanasubiri kuaga, tukaingia chumba maalum kwa huduma maalum ya kumuandaa jamaa! Dah kumcheki tu tukaona huyu sie kafa na hasira na maumivu hivyo uso na mwili vilikuwa vimekakamaa na alikuwa kama kajikunja

Tukajaribu kutumia mbinu zote tujuazo ili akae vema tumvalishe lakini ikashindikana tukaona anatuletea ujinga tukamletea ukauzu tukampa live kwamba hatujui hatumjui na tunafanya haya kwa ajili yake na watu wake hatulipwi chochote hivyo akiendelea kukomaa tutamvunjavunja viungo nguo ziingie!!! Mbona alilainika na tukamvisha fasta
 

Inawezekana kabisa japo ni kitu kibaya mno hii inatokana na uzoefu wa kazi anakuwa amehudumu muda mrefu kwenye sekta kiasi kwamba anakuwa na uwezo wa kusoma nyuso zinazokaribia kufa
 
Kuna vifo sio kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kuna watu hufa kwa vinyongo na visasi na wengine hufa ghafla huku wakiwa kwenye jambo moja muhimu sana! Hivyo hata baada ya roho kuachana na mwili bado ile conscious mind haitaki kukubali ile hali

Sasa mshana kwaninin akisimama usimwache uone mwisho wake unakua n nn!?
 
Sasa mshana kwaninin akisimama usimwache uone mwisho wake unakua n nn!?

Aende wapi wakati ameshathibishwa na daktari tena kwa maandishi kuwa kafa? Anataka kuwaletea watu skendo? Kwanini asingenyanyuka huko huko? Aende zake huko
 
Kuna mzee mmoja katika harakati za kutafuta life akajikuta ameangukia katika kazi ya kuwa mtu wa mochwari, kazi yake ikiwa
a.kupokea maiti mpya, kuzipanga chini kwqnza kablaa ya kuziweka kwenye mafriji.

b. Kutoa maiti zilizofatwa ili zikazikwe na wanandugu zao

c. Kuosha maiti kwa wale watao hitaji huduma hiii.

d. Kuzika maiti hasa za vichanga ambao ndugu zengine huwa hawaendi nazo kwa ajili ya mazishi.

e.pia anakuwa kama mlinzi wa maiti hizo, maana hufanya ukaguzi na kuzingalia kwa kipindi atacho kuwa hapo.

Huyu mzee kumbwa na mengi hata kupelekea kukimbia siku yake ya shift usiku, ila ngoja twende kwenye topic

haliwahi sema kuna strong willing ambayo watu wanakuwa nayo zinazofanya kuto kubali kufa, au kutotaka kufa kwa wakati huo, au kuna ambao waliweka nadhiri kwenye task au jukumu kuwa hawezi kufa hadi akamilishe, sasa mauti inapo mkuta hapo stil mindi na willing yake inakuwa hazijafa kabisa. Mara nyingi watu hawa huwa ni wanafanyiwa mchezo na wenzao.

Kuna kisa alikitolea mfano, Kuna mtu alikuwa anafanyaga mazoez daily, na yey husema lazima amalize round kadhaa ndio apumzke, sasa huyu mtu alipigwa kitu wakati wa mazoezi, akapelekew mochwari lakini alipofika kuna muda aliamka na kuzungumza kuwa ngoja nimalizie round 2 za mwisho, jamaa kaon mengj so hakuon na hajashangazw akamwambia nakusihi ufanye haraka, yule mtu akasimam aka kimbia mule rum, haoa na pale baada ya hapo aka nyoooka mazima, so similar case kama hizi hutokea zingine hazisemi zinafanya tu.

Pia akasema kuna strong will ya kukataa kifo baada ya kuona uchafu au madhambi aliyoyafanya kuwa ni mengi na kujua fika huko aendaki ni kubaya sana, hii hutokea hasa kwa wachawi au wauaji na majambazi sugu. Kuna bibi alifariki alipo pelekw pale baada ya kuumwa muda mrefu sana, majirani ndio waliokuw wanasaidia kuingiza mwili lakini kuna manen walikuw wakizungumza kuhusu skendo na tabia za marehem ikiwemo uchawi,

cha ajabu baada ya hao kutoka room yule bib wakati wanafunikwa vzuri usoni alimkamata muhudumu wa michwari akilalamika kuwa kwanini wanatoa siri zake, akisema anamwonyesh wote hadi yey, ila muhudum alimjib sasa umeshafariki baki na aman na manen mengine meng mengi akaachiwa bibi akajinyoosha.

Ila ishu kama mtu ukiwa na unfinished task ambayo ulikweka nadhiri kuwa utaifanya stil mind itakuwa conditioned kuwa active, dats why inasemekana duration inayochukua ubongo wa binadam kuganda au kufa ina tofautian after mauti kufika nahisi ishu ya kuwa determined kweny task fulan itaingia hapaa,
mshana jr
 

Safi sana merengo90 unajua mwili ukishapoa na pumzi kusimama moja kwa moja haimaanishi kwamba ile conscious mind nayo inakufa hapana ile ndio hubaki milele yani ni kama software ya binadamu
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…