Kuna watu Polisi wanajua kupindisha maelezo nadhani enzi za Hitler angewaajiri wamsaidie Joseph Goebbels kwenye kuandika propaganda!

Kuna watu Polisi wanajua kupindisha maelezo nadhani enzi za Hitler angewaajiri wamsaidie Joseph Goebbels kwenye kuandika propaganda!

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Yaani, katika kila tukio linalotokea, nadhani kuna watu huko Polisi ambao kazi yao ni kupindisha ukweli wa mambo kwa namna ambayo hata yule Joseph Goebbels, mkali wa propaganda wa Hitler, angewaonea wivu kwa namna ambavyo wanajua kupindua mambo!

Hebu angalia hili tukio la Mgombea wa Chadema kuuwawa huko Singida:

Mgombea wa Chadema auawa, askari Magereza mbaroni​

Jumatano, Novemba 27, 2024

1732708307617.png

Source: Mwananchi
Sasa angalia maelezo ya Polisi kuhusu kuuwawa kwa huyu mgombea
1732708369551.png

Source: Mwananchi

Unona basi; tukio limebadilika kutoka nyumbani kwa mgombea wa Chadema, na kwenda kwenye nyumba "moja". Na wavamizi wamebadilishwa kutoka wafuasi wa CCM na kuwa wafuaasi wa Chadema!

Kweli tuna Jeshi la Polisi! Inafikia mahali kuamini kinachosemwa na jeshi letu la Polisi ni sawa na mamba wa mto Masai Mara kuwaambia nyumbu ingieni mtoni tutawasaidia kuvuka na nyumbu wakaamini! Labda hao nyumbu ni sisi Watanzania!
 
Askari magereza asiye na jina?
Gereza lisilo na jina?
Mmoja akapigwa risasi lakini hakuna hata mmoja aliyekamatwa?
Watu wamefanya vurugu lakini hawajajeruhiana?

Wanasema, "unapokuwa muongo basi uwe na uwezo wa 'kufikiri'"
 
Askari magereza asiye na jina?
Gerezani lisilo na jina?
Mmoja akapigwa risasi lakini hakuna hata mmoja aliyekamatwa?
Watu wamefanya vurugu lakini hawajajeruhiana?

Wanasema, "unapokuwa muongo basi uwe na uwezo wa 'kufikiri'"
Kufikiri sio msamiati unaotumika kwenye jeshi la polisi Tanzania!

Polisi wetu ni waongo hadi ukiwaona barabarani unasikia kutapika!
 
Polisi wako busy wanaitengenezea maelezo hii hapa chini. Subiri uone itakavyotoka

1732712300256.png
 
Back
Top Bottom