Kuna watu sio wa kula nao ugenini aisee!

Raymanu KE

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2022
Posts
8,611
Reaction score
16,118
Wapo watu waliobarikiwa vipaji vya kufanya Mambo yao kwa speed ya pro max.Watu wa hivyo ukienda nao ugenini ikifika mida ya kula ole wako aisee!

Chakula kikiletwa mezani anatumia dakika Chache tu kuwahi kumaliza kula kabla wewe hujaanza kula vizuri ( hapa simaanishi mtu kumaliza chakula chote alichoandaliwa Wala siongelei ulafi)

Sasa umeenda na mwenzio ugenini ile mmeandaliwa chakula Cha pamoja tuseme ugali na kitoweo afu huyu jamaa yako anawahi kumaliza kula ghafla unamuona ananyanyuka kwenda kunawa anakuacha mezani upambane na chakula kilichobakia.

Naamini watu wengi wakiachwa mezani hivyo lazima na wao watasusa mlo hata Kama hawajafikia nusu ya kushiba coz hapa ukiendelea kula tu hata kwa dakika mbili lazima mwenyeji wenu ataanza kukuhisi vibaya eti wewe Ni mlaji sana au mlafi kidizaini [emoji23]

Ukute kitoweo chenyewe kilikuwa Ni mboga za majani mixer vipande kadhaa vya nyama afu jamaa ulianza kula mboga kwanza vipande vya nyama vitakuwa vya mwisho( wengi tuna hii tabia).Sasa kiherehere Cha rafiki yako( eti amejifanya ameshiba baada ya kula kidogo) kinaweza kukufanya ukavisusa hivyo vipande vya nyama ambavyo uliplan kuvila mwishoni[emoji26]

Nikushauri tu kamwe usijaribu kwenda ugenini na mtu anayependa kuwahi kumaliza Mambo yake kabla yako maana huyo atakuzingua mida ya kula.Atafanya ususe chakula wakati hujashiba eti ili uende sambamba naye.
Yalinikuta siku Moja haya[emoji23]
 
Mkuu unakuwa na aibu kwenye, Aiseeh kweny Mambo yote nitadelay lkn co kweny msos utavyonfklia ndo Ivo ivo
 
RAHA JIPE MWENYEWE ANASEMWA MBUZI ANA MKIA MFUPI NA BADO ANAKULA MAJANI KWA RAHA ZAKE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…