Kuna watu wakarimu dunia hii

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Wiki iliyopita nilisafiri kwenda Tanga, nilipanda basi la Raha Leo. Pembeni yangu alikaa mwanaume amenizidi miaka kama 10 hivi. Nilikuja kugundua baadae ni m-Pakistan na Kiswahil aliongea kidogo sana.
Jirani yangu huyu alikaa siti ya dirishani. Alikuwa amejiandaa kweli kwa safari. Alikuwa na mfuko wa makula kula. Kwenye mfuko alikuwa na meat chops, biscuits, chocolate, juice.

Tulipifika Chalinze nilimuomba aninunulie korosho kwani yeye alikuwa amekaa dirishani, ndipo nilipogundua uwezo wake wa lugha ya Kiswahili.

Alipoanza kutoa vyakula, alinikaribisha meat chops, nilijibu asante, kabla ya kutoka nyumbani nilipiga breakfast ya nguvu na nilijua lunch ya ugali na mchunga inanisubiri kwangu mimi korosho zilitosha.

Baba huyu roho yake ilisononeka sana kwa kukataa kwangu kula chakula. Alinipa chocolate, ilibidi niichukue kumridhisha.

Aliniacha hoi, alipofungua box la juice na kuniambia nianze kunywa mimi kwani anajua akianza yeye mimi sitakunywa. Nilimuomba kuwa mimi ni mzima, nilikuwa na chupa ya maji nikamionyesha huku nikimfahamisha kuwa ninapunguza matumizi ya sukari, kwangu mimi maji ndiyo mpango mzima.

Huu ni Mfano wa gentleman ambao wamebaki wachache sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…