Kuna watu wana majina kutoka kwa MIZIMU!

Kuna watu wana majina kutoka kwa MIZIMU!

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,277
Reaction score
8,860
Ni vizuri kuelewa jina lako au la mtoto na maana yake, kuna mambo mengi hukutokea kwa uzuri au ubaya lakini yawezekana na jina lako linachangia au asili ya jina lako …

Kuna wengi wetu wamepewa majina yao kutoka kwa mababu zao ambao walikua na roho fulani labda ya umasikini, uzinzi, magonjwa n.k. Wengine wamepewa majina kutoka kwa waganga wa kienyeji au mizimu, ndio maana kuna vifungo fulani unavyo kwenye maisha yako.

Jina lako linang’ang’ania ubaki pale pale, hakuna kusonga mbele, wewe ni wa hivyo hivyo au unajimilikisha magonjwa fulani kwasababu bibi au babu zako walikua nayo.

Mfano unasema mimi ugonjwa wangu ni kisukari, TB au sie kwetu ndio ugonjwa wetu! nk

Tukatae misingi mibaya ya majina yetu, tusikubali wala usikubali kumpa mtoto wako majina ya laana

Kwa mfano Shida,Matatizo,Makusudi n.k.

Ni vizuri kukubali au kuwapa watoto majina yenye baraka na kibali katika maisha yetu.

Barikiweni sana!
 
Thread ya June 12, 2014. Wachangiaji wanne?

Yote haya yanategemeana na imani yako. Ukimwamini Mungu kwa moyo wote na ukaliita jina la Yesu kwa imani kabisa kabisa hata kama una laana za mizimu mabilioni zote zinapukutika. Ni hayo tu kwa sasa....
 
Hakuna waarabu wanaowacheka waarabu wenzao sababu wana majina ya asili ya kiarabu kama abdallah,Fatima,sabrah,Mohammed au hata kusikia wazungu wakidhihaki wazungu wenzao kisa wana majina ya kiasili ya kizungu kama john,james,happiness,bless,loveness lakini wapo waafrika wanaotumia majina ya asili ya kizungu na kiarabu wanawacheka waafrika wenzao wenye majina ya asili ya kiafrika.

Dah
 
Ndio maana akina john na maimuna wamekuwa wengi, Yale majina yetu tunaita ya mizimu

Buree
 
Thread ya June 12, 2014. Wachangiaji wanne?

Yote haya yanategemeana na imani yako. Ukimwamini Mungu kwa moyo wote na ukaliita jina la Yesu kwa imani kabisa kabisa hata kama una laana za mizimu mabilioni zote zinapukutika. Ni hayo tu kwa sasa....
Ilikuwa imefichwa nikaifichua

Sent from my INFINIX-X551 using JamiiForums mobile app
 
Thread ya June 12, 2014. Wachangiaji wanne?

Yote haya yanategemeana na imani yako. Ukimwamini Mungu kwa moyo wote na ukaliita jina la Yesu kwa imani kabisa kabisa hata kama una laana za mizimu mabilioni zote zinapukutika. Ni hayo tu kwa sasa....
hahahhha Mshana jr ndie kaifukunyua ilipokuwa, inaonekana tokea alivyopost haikupata mchangiaji hadi leo Mshana jr alivyoichokonoa
 
Kuna majina ya asili kama bashite yaani ni zuri hata kutamka.

Kiukweli napenda sana majina ya asili na pia najivunia kupewa jina la asili
 
Back
Top Bottom