konda msafi
JF-Expert Member
- Sep 5, 2018
- 1,696
- 8,763
Kuna watu wana hoja mfu sana. Wanabeza Rais kusikiliza maneno ya mtandaoni. Kwani watu walioko mitandaoni sio watanzania au hawapaswi kusikilizwa? Watu wa mitandaoni ndio hawa hawa watu wa mitaani. Au wanadhani watu wa mitandaoni wanatoka sayari nyigine?
Mitandao ni platform sahihi kabisa ya watu wa kawaida kutolea maoni yao, na Rais kama kiongozi wao yupo sahihi kabisa kuyafanyia kazi maoni ya kwenye mitandao maana yametolewa na raia wake ambao hawana uwezo wa kumfuata ikulu na kuongea naye ana kwa ana.
Raia wa kawaida hawana uwezo wa kuonana na Rais kwa urahisi hivyo mitandao ni sehemu pekee ya kuwasilisha malalamiko yao. Na nadhani Rais wetu analitambua hilo ndio maana amekuwa akisisika akiongelea anachokisoma mitandaoni.
Hao wote wanaobeza Rais kusikiliza maneno ya mtandaoni nadhani wana matatizo yao binafsi au kuna maslahi yao yanaguswa. Wanataka Rais asisikilize maneno ya mitandaoni halafu asikilize maneno ya wapi ilihali hata wabunge wetu hawatusemei huko bungeni kazi kujipendekeza na kusifiasifia tu kusikokuwa na faida yoyote kwa raia wa kawaida.
Mama Samia njia uliyoichukua ya kusikiliza maneno ya mitandaoni ni sahihi kuliko maelezo yenyewe maana hawa watu wa mitandaoni ndio raia wanaokutegemea uwatumikie kupitia dhamana uliyo nayo na mitandao ndio njia yao pekee ya kukufikishia ujumbe wao maana hawana uwezo wa kukufuata ikulu.
Kazi iendelee.