robbyr
Senior Member
- Apr 8, 2017
- 129
- 221
Kuna dharau ila hii inavuka mpaka!!
Kuna watu wanaleta utamaduni wa hovyo wa kutukana viongozi wa nchi. Ndugu zangu hiyo sio demokrasia ya midomo.
Hata waliotuaminisha hayo kwenye nchi zao sijawahi kuona kiongozi anatukanwa kiasi hiki.
Marekani hii kitu haipo( wanakosoa kwa staha si matusi kwa kiongozi). Je, tunafundisha nini kizazi kinachokulia mtandaoni? Kwamba kukosoa ni kutukana.
Mpaka sasa naanza kusikia chuki za kidini na kikanda kutoka kwenye vinywa vya viongozi tulioona wana akili.
Basi tu, mna kiongozi mpole na anayejua kupuuzia mambo ila nitakubali kukosolewa ila si kudhalilishwa wala kutukanwa.