Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Mdude na wenzake wanaishi Mbeya; wamekaa Mbeya toka hukumu ya DP world ilipotolewa na wakatoa na matamko yao hakuna aliyewakamata.
Mara paap wamepanga safari waje zao kula bata mjini wanakamatwa usiku wa manane Mikumi; kisha utasikia wamepelekwa makao makao makuu Dodoma mara wamepelekwa Mbeya. Huku kote wapo watu wamejiwekea hivi kama justification ya posho
Wakimaliza kulipwa naamini wataachiwa; sina namna nyingine ya kueleza hiki kinachotokea kama siyo watu kutafuta posho.
MDUDE kichwa imepinda ile unamhoji nini? Huyu ni mwanasiasa, wakili aliyepeleka kesi mahakama pia ni mwanasiasa. Anazungumza hoja za kisiasa then kwanini utumie mafuta na posho kuangaika nao?
Kwa mfano wangepewa wito pale Mbeya waripoti polisi wasingeripoti? Mnaopanga haya mambo mnamfanya Mhe. Rais aonekane kama anawanyanyasa hawa watu bure.....kweli mtu wakumwandikia barua au kumpigia simu afike ofisini una haja ya kumvuzia usiku wa manane?
Mnapat raha gani kila siku vyombo vya kimataifa kusema wanasiasa wa upinzani mara wanasheria wakamatwa? Katika mazingira haya mnadhani wawekezaji serious watakuja nchini? Mnadhani wakija watakubali fedha zao zibaki ndani ya nchi au watakuwa wanahamisha fedha kila siku? Wakihamisha fedha na kupunguza kuwekeza ndani dola ntapata wapi?
Let us invest kwenye economic intelligence; tuache kuwaza uchaguzi kila saa. Tufanye shughuli za uchumi kusubiri 2025