Kuna wazazi wangapi wasomi hapa Tanzania wanaolea mtoto kama ambavyo huyu binti anavolelewa ?

MELEKAHE

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2023
Posts
2,230
Reaction score
8,337
binti wa miaka saba akiwa anakamua maziwa kwenye ngombe wa nyumbani kwao

Your browser is not able to display this video.



binti akiwa bandani anafuga zake kuku




Your browser is not able to display this video.
 
Huyo ukubwani akija pata pesa hawezi kubali mwanae ateseke kama yeye hivyo

kwani hapo anateseka ?, kwao kuna kila kitu ambacho tunaemuita tajiri hapa Tanzania anacho, nyumba nzuri, magari yapo, mifugo ipo.

kukamua ngombe ni kazi yake huyo binti kila siku jioni, asubuhi tu ndio hakamui sababu anaenda shule asubuhi


Your browser is not able to display this video.
 
Mateso ambayo huyaoni sio kazi hio ya kujivunia kwa mtoto. Nawaunga mkono wasomi wasiowafanyia watoto wao hivyo.
 
Mtoto afundishwe vingine aiseee sio hio kukamua ng'ombe halafu baadae awe wale 50/50 aanze kulaumiwa na jamii kwa kutetea haki zake
Kukamua maziwa kwa ng'ombe si mateso cute....ni maisha tu kama tuendavyo kazini ili tushibe
 
Bongo wanaamin kumuhusisha mtoto kwenye makazi magumu ndo kumlea,

M mwanangu nataka awe Dr, au computer scientist, nitamtunza na kumpeleka sehemu hizo akajifunze
 
cha kushangaza huyo binti anafurahia hiyo kazi, na binti anaekamua ngombe anatoka familia mambo safi kuliko huyo anaeona binti anateswa
kuna mjinga moja aliwahi nambia eti natesa watoto kwa kuwambia wafagie wanja asubui kabla hawajaenda shule na kuhakikisha vyumba vyao viko safi

sasahivi naona anaelewa nini maana yangu baada ya miaka mingi kupita
 
binti wa miaka saba akiwa anakamua maziwa kwenye ngombe wa nyumbani kwao

View attachment 3299317


binti akiwa bandani anafuga zake kuku




View attachment 3299318
Wa-Brazil waache na lifestyle yao, umeona kipande kidogo cha vijikazi vya hapa na pale na lengo ni wewe uone, ukiona cycle nzima ya watoto wa Brazil utalalamika kwamba malezi yao ni kinyume na 'maadili' yetu.
Hata wewe unaweza kurekodi watoto wako vitu selective vya kusifiwa na utaonekana ni mzazi anayepaswa kuigwa.
 
Kuna ugumu wowote kwa mtoto wa umri huo kukamua ng'ombe kwenye familia ya wafugaji? Pia kuna ugumu gani kwa mtoto kama huyo kukaa kwenye kundi la kuku au mifugo mingine yoyote, kupiga nayo picha na kuzirusha mitandaoni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…