Kuna wazee wana hekima na busara sana

CARIFONIA

JF-Expert Member
Joined
Aug 17, 2013
Posts
616
Reaction score
1,453
Nilimuuliza rafiki yangu ambaye amevuka miaka 70 na sasa anakwenda kuelekea miaka 80, ni mabadiliko gani amehisi ndani yake? Alinitumia yafuatayo:

1. Baada ya kuwapenda wazazi wangu, ndugu zangu, mwenza wangu, watoto wangu, na marafiki zangu, sasa nimeanza kujipenda mimi mwenyewe.

2. Nimetambua kuwa mimi si "Atlas." Ulimwengu haupo mabegani mwangu.

3. Nimeacha kubishana bei na wauzaji wa mboga na matunda. Sentensi chache zaidi haziwezi kuniumiza, lakini zinaweza kumsaidia muuzaji masikini kuokoa kwa ajili ya ada ya shule ya binti yake.

4. Ninamwachia mhudumu wangu wa mgahawa bakshishi kubwa. Pesa hiyo ya ziada inaweza kumletea tabasamu. Anajitahidi sana kuishi kuliko mimi.

5. Nimeacha kuwaambia wazee kuwa tayari wameshasimulia hadithi hiyo mara nyingi. Hadithi hiyo inawafanya wapitie kumbukumbu zao na kuishi upya maisha yao ya zamani.

6. Nimejifunza kutojishughulisha na kurekebisha watu hata ninapojua kuwa wamekosea. Si jukumu langu kuwafanya watu wote wawe wakamilifu. Amani ni ya thamani zaidi kuliko ukamilifu.

7. Natoa pongezi bila hiyana. Pongezi ni tiba ya hisia sio tu kwa mpokeaji, bali pia kwangu. Na kwa mpokeaji wa pongezi, kamwe, KAMWE usikatae pongezi, sema tu "Asante."

8. Nimejifunza kutojali kuhusu mikunjo au doa kwenye shati langu. Haiba inaongea kwa sauti zaidi kuliko muonekano.

9. Naondoka mbali na watu wasionithamini. Wanaweza wasijue thamani yangu, lakini mimi najua.

10. Nakaa tulivu mtu anapocheza rafu kunizidi kwenye mbio za maisha. Mimi si panya na wala sipo kwenye mbio yoyote.
11. Ninajifunza kutoona aibu kwa hisia zangu. Ni hisia zangu zinazofanya niwe mwanadamu.

12. Nimejifunza kuwa ni bora kuacha kiburi kuliko kuvunja uhusiano. Kiburi changu kitanitenga, lakini kwa mahusiano, sitakuwa peke yangu.

13. Nimejifunza kuishi kila siku kana kwamba ni ya mwisho. Mwisho wa yote, inaweza kuwa kweli ya mwisho.

14. Ninafanya kile kinachonifurahisha. Ninawajibika kwa furaha yangu, na nina deni hilo kwa nafsi yangu. Furaha ni chaguo. Unaweza kuwa na furaha wakati wowote, chagua tu kuwa nayo!

Nimeamua kushiriki haya kwa marafiki zangu wote. Kwa nini tusisubiri kufikia miaka 60 au 70 au 80? Kwa nini tusianze kuyatenda haya katika umri wowote?
 
Rafiki yako anaelekea umri wa miaka 80 ndio anakumbuka shuka wakati kumekucha?

Anyway kua na rafiki wa 80 years old,bila shaka na wewe umri umesonga.
 
SIPENDI SIASA Ramon Sanchez
 
Sure hizo ndio hekima za utu uzima ukiwa nazo ungali kijana basi wewe utafanikiwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…