Kuna Wizara ya Afya, Wizara ya Ustawi wa Jamii, Watoto, Jinsia na Walemavu wao wanafanya kazi gani ikiwa Makonda ndio anasaidia wahitaji?

Kuna Wizara ya Afya, Wizara ya Ustawi wa Jamii, Watoto, Jinsia na Walemavu wao wanafanya kazi gani ikiwa Makonda ndio anasaidia wahitaji?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Anajua kazi ya Wizara ya Ustawi wa Jamii,Jinsia, Walemavu na Watoto aniambie maana naona Makonda Toka akiwa Mwenezi alikuwa anafanya hii kazi.

Wao wanaliowa Mishahara Kwa kaiz hizo na hawafanyi Sasa wanalipwa Kwa Ajili ya nini hasa? Yaani Wameshindwa kuratibu na kujua watu wenye uhitaji hasa Watoto wadogo na Walemavu Ili Serikali itenge Bajeti ya kuwasidia?

Wizara nyingine ni za kufuta tuu Kwa sababu hakuna Cha maana wanafanya,wapo Hadi Maofisa Ustawi wa Jamii lakini uje umuulize anajua hata idadi ya Walemavu kwenye eneo lake?

Kimsingi tuna kundi kubwa la Utumishi wa Umma ambao hawajielewi wanachofanya.

---

Mkuu wa Mkoa wa Arusha ametoa Viti mwendo viwili, Bima za afya tatu na Mitaji ya milioni sita kwa kinamama watatu wanaolea watoto wenye ulemavu na wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali mkoani Arusha.

Mhe. Makonda ametoa msaada huo leo wakati akiwa Mjini Arusha kwenye viwanja vya Ngeresero mara baada ya kupata maombi ya msaada huo kutoka kwa Kinamama hao ambapo wamekuwa sehemu ya mamia ya wakazi wa Arusha waliosikilizwa na kutatuliwa kero zao mbalimbali na Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na ofisi yake.

Wazazi wa watoto hao wamemueleza Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Christian Makonda changamoto za watoto wao ambao wengi wao ni watoto yatima huku wakiishi na mama zao ambao wamekuwa wakiishi kwa utegemezi kutokana na kukosa ajira.

"Ni changamoto ambazo zinatokea na ni kama majaribu vile ya dunia, kwahiyo niwaombe msiwatupe watoto. Hii ni mitihani tu ambayo binadamu anapitia kwahiyo naomba msiwatupe watoto. Msifanye hilo kosa.", amesema Mhe. Makonda.

Mkuu wa Mkoa ameendelea na ziara yake kwenye wilaya mbalimbali za Mkoa wa Arusha ambapo amekuwa akisikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi kwenye mikutano yake ya hadhara ikiwemo kero binafsi ambazo nyingi zimekuwa zikihusisha magonjwa na wengi kushindwa kugharamia huduma mbalimbali ikiwemo za matibabu.
 
Watumishi wa taasisi wanajua kinachoendelea?
Wanajua wakianza na Waziri wao ila ndio hawajitambui unategemea watafanyaje?

Kwanza Huwa nashangaa yaani Wizara ya Ustawi na Afya zinashindwa kujua idadi ya Watoto walemavu,na wenye mahitaji maalumu wawatambue Ili Serikali itenge pesa? Wamewaachia wazazi wenye Watoto wengi wao hawana uwezo ndio hao wanamuona Makonda ni shujaa wao
 
Safi sana mkuu. Hii ni hatari sana pale system inapotegemea ma superstar leaders kama Makonda badala ya kuwa na mfumo maalum wa uongozi. Hii ni sio hali nzuri kabisa.
CCM ni kama timu ya mpira iliyozidiwa mbinu, kwa sasa inategemea vipaji vya wachezaji mmoja mmoja kuwavusha infact ndio utaratibu wao. Corrupted system.
 
Back
Top Bottom