Kuna wizi umetokea banki

madeinmusoma

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
324
Reaction score
387
Jambazi "wote laleni chini pesa ni za serikali na
maisha ni ya kwenu", wote wakalala chini HII
INAITWA DHANA ...YA USHAWISHI - kubadilisha
njia ya kawaida ya kufikiria.

••••••••••••••••••••
Kuna dada kwa woga akawa amelala chini
kimitego, Jambazi akamwambia, "dada hebu
kuwa na adabu chukua kanga jifunike hili ni
tukio la ujambazi na sio la ubakaji.” HUU
UNAITWA WELEDI - zingatia ulichofundishwa
kufanya

•••••••••••••••••••••••

Walipotoka kwenye wizi jambazi mdogo ambaye ana shahada ya uzamili ya biashara akamwambia mwenzake, "tuzihesabu hizi fedha.” Yule mkubwa akamcheka kwa dharau na kumjibu, "wewe mjinga sana hizo hazina haja ya kuhesabu saa mbili
watatutangazia kwenye taarifa ya habari tumeiba
kiasi gani. HUU INAITWA UJUZI - Siku hizi ujuzi
ndio bora kuliko vyeti

•••••••••••••••••••••••

Baada ya majambazi kuondoka meneja akamwambia mhasibu wa bank, " ujumlishie na zile milioni 80 tulizo iba sisi.” HUKU KUNAITWA KUOGELEA NA MKONDO WA MAJI - kushabihiana na mazingira magumu kwa faida binafsi.

•••••••••••••••••••••••

Mhasibu akafurahi na kusema, "dah wizi ukitokea kila mwezi itakuwa burudani sana.”

HUKU KUNAITWA KUWA NA MAWAZO CHANYA -
Furaha ndio kitu cha muhimu zaidi

•••••••••••••••••••

Meneja kafurahi sana kwa kuwa sasa matatizo yake yametatuliwa na wizi uliojitokeza.
HUKU KUNAITWA KUTHUBUTU- shikilia nafasi pale inapojitokeza hata kama ni hatari kiasi gani.

•••••••••••••••••••••••

Haya usiku wake taarifa ya habari ikatangaza kuwa wizi mkubwa sana wa million 100 umetokea leo benki. Majambazi kusikia hivyo wakaanza kuhesabu zile pesa lakini wakajikuta na milioni 20 tu. Yule jambazi mkubwa akashituka na kusema, "dah! yaani meneja kaiba mara nne zaidi yetu bila
kuchezesha msuli? Bora umeneja kuliko ujambazi.”

HII INAITWA ELIMU NDIYO KILA KITU

Ishike sana elimu ina nguvu kuliko adhabu.
 
[emoji1732][emoji1732][emoji1732]
 
Kumbe mijambazi wanaifuga humohumo benki..
 
Huyo mrembo alieambiwa ajifunike kanga alikuwa kajibenua nini maana jambazi pia kaona kirumbua chahitaji kufunikwa
 
Yaaah ni chemsha bongo nzuri na maridhawa, asante sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…