Kuna wizi umetokea benki

GANG MO

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2016
Posts
2,092
Reaction score
2,210
KUNA WIZI UMETOKEA BENKI
••••••••••••••• •••••••
Jambazi akasema "wote laleni chini pesa ni za serikali na maisha ni ya kwenu",
wote wakalala chini (HII INAITWA
DHANA ...YA USHAWISHI - kubadilisha
njia ya
kawaida ya kufikiria).

Kuna dada kwa woga akawa
amelala chini kimitego, Jambazi
akamwambia, "dada hebu kuwa
na adabu chukua kanga jifunike hili ni tukio la ujambazi na sio la
ubakaji.” (HUU UNAITWA WELEDI -
zingatia ulichofundishwa kufanya)

Walipotoka kwenye
wizi jambazi mdogo ambaye ana shahada ya uzamili ya biashara akamwambia
mwenzake, "tuzihesabu hizi fedha.” Yule mkubwa akamcheka kwa dharau na kumjibu, "wewe mjinga sana hizo hazina haja ya
kuhesabu saa mbili wata tutangazia kwenye taarifa ya habari tumeiba kiasi gani. (HUU INAITWA UJUZI - Siku hizi ujuzi ndio bora. kuliko vyeti)

Baada ya majambazi
kuondoka meneja akamwambia mhasibu wa bank, " ujumlishie na zile milioni 80 tulizoiba sisi.” (HUKU KUNAITWA
KUOGELEA NA MKONDO WA MAJI -
kushabihiana na mazingira magumu kwa
faida binafsi.)

Mhasibu akafurahi na kusema, "dah wizi ukitokea kila mwezi itakuwa burudani
sana.” (HUKU KUNAITWA KUWA NA
MAWAZO CHANYA - Furaha ndio kitu cha
muhimu zaidi)

Meneja kafurahi sana
kwa kuwa sasa matatizo yake
yametatuliwa na wizi uliojitokeza. (HUKU KUNAITWA
KUTHUBUTU-shikilia nafasi pale
inapojitokeza hata kama ni hatari kiasi
gani.

Haya usiku wake taarifa ya habari ikatangaza kuwa wizi mkubwa sana wa million 100 umetokea leo benki. Majambazi kuskia hivyo wakaanza
kuhesabu zile pesa lakini wakajikuta na milioni 20 tu.
Yule jambazi mkubwa akashtuka na kusema, "dah! yaani meneja kaiba mara
nne zaidi yetu bila kuchezesha msuli? Bora umeneja kuliko ujambazi.” (HII INAITWA
ELIMU NDIYO KILA KITU - ishike sana
elimu ina nguvu kuliko chochote.)

������������������
 
Nimefatilia kwa kina nikajua benk leo kumenuka kumbe simulizi. Asante
 
Umeenda vizuri tu ila hapo mwisho ndo umeharbu!au itakuwa hii story ya kitambo enz za mkapa kurudi chini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…