Ninapata mashaka na mifumo ya control number huenda imechezewa sana. Katika hali ya kushangaza, mifumo hii ina tabia za kutofautiana sana kutoka taasisi moja hadi nyingine na ndani ya taasisi moja.
Nitatoa mfano;
Nilikuwa nadaiwa pesa yapata laki nne nikapewa control number. Hata hivyo nilitaka kuzilipa kwa awamu mbili, lakini mfumo ulinilazimisha nilipe pesa yote kwa wakati mmoja.
Siku nyingine nilitakiwa kulipa laki na elfu sitini, hata hivyo kwa haraka zangu nilijikuta nimelipa online kupitia benki kiasi cha laki moja na nusu. Nikasubiri majibu kuwa nimelipa, lakini haikunipa majibu yoyote. Nikaenda benki wakaniambia pesa imekatwa na kulipa hiyo pesa lakini control number bado inaonekana haijapokea malipo.
Kwa vile ilikuwa na deadline, niliamua kulipa kupitia njia ya tigo pesa halafu nikawadai benki ile pesa waliyokata kwenye akaunti yangu. Wao wakasema nao wanaidai kwenye taasisi iliyoikata pesa hiyo. Ni mwezi wa tano leo sijaipata pesa hiyo.
Pia kuna wakati nilipigwa faini barabarani kwa kuzidisha spidi ya gari. Nilivyoandikiwa control number, ilionesha jina la mmiliki wa awali wa gari, wakati nilishabadili umiliki TRA. Nilijiuliza kwa nini mifumo hii haisomani? Au kuna kitu kipo nyuma ya pazia hatukijui?
Nashawishika kuamini kuna hujuma kubwa sana inafanywa kwenye hii mifumo na huenda kuna vigogo wa siri hii.
Kwa hali ilivyo, ni Rais pekee ndiye anaweza kufanya kitu. Badala ya kuagiza wanaosimamia mifumo hii wachunguze, anapaswa kuagiza watu wa usalama wa taifa wafanye kazi hiyo. Ikibidi watafute wataalamu wa nje kama vile Israel kuwasaidia. Vinginevyo watu watakuwa wakitakatisha pesa tu na hatuwezi kuwajua.
Pia soma: DOKEZO - Serikali inapata hasara ya mabilioni kwa watumiaji wa mifumo ya TEHAMA kulipia huduma isiyoendana na kiasi cha fedha kilicholipwa