Kuna Yanga halafu kuna timu za Ligi Kuu

Makonyeza

Member
Joined
Feb 2, 2020
Posts
72
Reaction score
261
Kuna YANGA halafu kuna timu za Ligi kuu:

Achana na ukubwa wa soka tunalocheza Sasa na matokeo ya mechi ya Jana dhidi ya Azam,
Kila mtu anasema lake, acha na mimi nichangie, lakini kwa kuanzia naomba kusisitiza kwamba kwenye ligi yetu kuna YANGA halafu kuna timu shiriki za Ligi Kuu.

Kaka yangu Oscar Oscar nimemsikia anasema tena kwa kijiamini kabisa eti Yanga inadekezwa sana kwa kuachwa ifanye inavyotaka kwa lile Sakata la rangi ya nembo ya Mdhamini, halafu akatolea mfano eti itakuwaje na kina Mtibwa, Namungo, Coast na wengine nao wakija na masharti Yao?

Oscar anaenda mbali zaidi anastaajabu eti Yanga inayojiandaa kwenda kwenye mabadiliko kujiendesha kibiashara inakuwaje inakuja na vikwazo kwa mdhamini.

Lakini sio huyo tu, Kuna rafiki yangu anaitwa Yeriko Nyerere, eti naye anakesha kupambana na Yanga kwenye mitandao akidai kutetea kanuni za Ligi kuu.

Hawa wote wanaojiita wachambuzi wanatumia nguvu kubwa kutushawishi eti NBC wamesaini mkataba na TFF na sio Yanga, hii hoja mfu kabisa na sikutegemea kutoka kwenye vinywa vya baadhi ya wanaojiita waandishi na wachambuzi wa michezo, kumbe huwa tunawasikiliza watu wenye upeo finyu sana wa mambo ya michezo.

Na Kaka yangu Mwenyekiti wa bodi ya Ligi Kasongo Diamond naye akajitokeza kusisitiza kuhusu kanuni akiambaa humo humo.

Sasa iko hivi, Yanga wala haidekezwi, Yanga wala hawavunji kanuni za Ligi, bali Yanga wanajitambua, yes wanajitambua.

Wakati Tff wakisaini mkataba na NBC walijua wana Yanga yenye katiba utamaduni na miiko yake kama ilivyo kwa timu zingine.

Ni ukoloni pekee na utandawazi ndivyo vimeathiri miiko na tamaduni zetu wa Afrika lakini nao haukuweza kutubadilisha uafrika wetu, seuse NBC kwa Yanga.

NBC anahitaji kufanya biashara na Yanga, Yanga hajakataa, amekubali kupita TFF ila ana haki ya kutoa masharti yake ili kulinda maslah yake iwe kitamaduni kama inavyosemwa au kiuchumi.

Yaani isidhaniwe mdhamini akija Tff anakubaliwa tu, lazima clubs ambazo ndio wadau wakuu washirikishwe na waridhie, Tff yeye ni msimamizi tu wa Mpira, Tff hana timu wala hachezi Mpira. Yeye Tff anazitegemea hizi timu kufanya biashara.

Hivi umeshajiuliza what if Yanga au Simba wangekuwa wanadhaminiwa na Bank yoyote nyingine mbali na NBC, Simba na Yanga wangekubali kuitangaza NBC, jibu ni hapana na pengine ingekuwa kwa masharti magumu sana ambayo NBC isingevumilia.

Sasa Yanga inajengwa na utamaduni na kusimamia na katiba yake ambayo haviruhusu rangi nyekundu kwenye mambo Yao, hakuna kinachoweza kuibadilisha hili kwa haraka haraka hivyo.

Tff anakuhitaji Yanga/Simba zaidi kuliko Tff, coz Tff haina mashabiki, hili mbona jepesi tu. Kenya wenzetu kwao Mirungi ni halali, Jamaica kwao Bhangi ni halali, hivi waje tu kwetu kwamba wanataka wafanye biashara na Tanzania basi ndio tuwaruhusu waje wauze mpaka hizo biashara haramu kwetu, jibu ni hapana.

Oscar Oscar amepanga nyumba ya biashara kwa Sheikh Kitenge basi asiambiwe kwamba a naruhusiwa biashara zote isipokuwa Pombe na kitimoto?

Yes, tunahitaji kwenda kwenye mabadiliko tume fungua Milango na Madirisha kuruhusu hewa Safi(mabadiliko) haimaanishi tusiweke wavu(masharti)kuzuia mbu na wadudu wengine hatarishi.

NBC anajua anawahitaji YANGA(tuseme na Simba) ndio sababu kaja Ligi kuu vinginevyo angeweza kwenda zake Zanzibar pia kuna Ligi kule au angeenda kudhamini FDL Kuna timu pia kule lakini hakuna YANGA inayokuhakikishia Mamilioni ya Mashabiki ambao ndio walengwa kwenye mkataba wa NBC.

HIVI mliwasikia Vodacom wakati wakitoa sababu za kutoendelea na mkataba na Tff, walieleza kwamba wamepata hasara kwa sababu kadhaa, kati ya sababu zilizotajwa Yanga au matumizi ya Nembo isiyokuwa na rangi nyekundu ilitajwa.

Kibiashara mdhamini hata Yanga hawahitaji, anachohitaji yeye ni mashabiki wake hata wale wa timu pinzani ambao watakuja uwanjani, Yanga yeye ni njia tu ya kuwapata hao wananchi, Oscar Oscar na Yeriko Nyerere mpo?

Hizo kanuni zimewekwa ili watu wacheze Mpira, na wala hatuchezi Mpira ili tuwe na kanuni[emoji12].
Yanga/Simba ni kubwa kwelikweli kuliko hao TFF na hao wadhamini pia.

Kwani hamuoni, Azam Media juzi wamesaini mkataba wa mabilioni na Yanga, achilia mbali ule na Tff, ile inatosha kukuthibitishia kwamba kuna YANGA yenye watu na kuna TFF, ebu kuweni na heshima basi, yaani Yanga uitolee mfano kuifananisha na Biashara au Namungo kibiashara?

Majaliwa M.
 
Kwa hiyo mzee wa ujasusi wa kidola naye kumbe ni kopo tu kama yale makopo mengine! Uchambuzi murua kabisa. Ungekuwa jirani, haki ya nani ningekupiga na kipogo kimoja cha mnazi kudadeki.

Maana umenifurahisha sana.
 
Hao jamaa ni wapuuzi tu,yanga watasikilizwa maombi Yao na hakuna kitu wanaeza fanya
 
hawa yanga wangekua wanagoma kuvaa ile nembo ya total kule caf ambayo ina rangi nyekundu ningesema kwel wanasimamia tamaduni ila kwa kugoma kwao kuwagomea tff tu basi lazima tukubali tff inaviogopa hivi vilabu
 
hawa yanga wangekua wanagoma kuvaa ile nembo ya total kule caf ambayo ina rangi nyekundu ningesema kwel wanasimamia tamaduni ila kwa kugoma kwao kuwagomea tff tu basi lazima tukubali tff inaviogopa hivi vilabu
Yanga na Simba ndio mpira wa Tanzania, bila moja wapo hakuna soka Tanzania elewa hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…