Kuna yapi ya kuzungumza zaidi ya mpira? Mpira wa miguu ni uraibu mpya unaoongezeka kwa kasi

Kuna yapi ya kuzungumza zaidi ya mpira? Mpira wa miguu ni uraibu mpya unaoongezeka kwa kasi

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Nchi yetu sasa imeingia rasmi katika ulimwengu wa uvuvuzela wa mpira. Kama vile ulivyo uraibu wa pombe, ngono, sigara n.k Idadi kubwa ya raia wa nchi kwa sasa wanalala wanazungumza mpira, wanaamka wanazungumza mpira na wanashinda wanazungumza mpira.

Bahati mbaya sana mpira wenyewe ambao haukauki midomoni ni mpira wa Liverpool, Arsenal, Man United n.k na sio mpira wa Namungo, Dodoma jiji, Ruvu Shooting na timu nyinginezo wenyeji kutoka miji wanayoishi raia wenyewe.

Wenye ajira nzuri, wamachinga, wasio na ajira, walalahoi, waliopigika, wanaoujua mpira, ambao hawaujui na wanaojifanya kuujua mpira wote content kubwa kila siku ni Liverpool, Chelsea, Simba na Yanga.

Hatuna mambo mengine tunayoweza kuyazungumza na kuyafanya makubwa na muhimu kama mpira?
 
Hili suala mimi nilifikri ni peke yangu tu ndio naona!

Yani watanzania sasa hivi mada yao kubwa ni moja tu mpira basi.

Zamani tulikuwa tumezoea sisi wanaume ndio tunaojadili sana mambo ya mpira ila cha ajabu hata wanawake siku hizi mnatoka ngoma draw mkianza kubishania mpira.

Ndio maana sasa hivi kuna mambo mengi ya kijinga yanayopita huko selikali huwezi kuona yakiibuliwa na yeyote na hata akitokea mtu akiibua ufisadi sehemu watu wanachukulia poa tu. Mfano ni lile suala la mtu kujiunganishia bomba la mafuta yaani lilikuwa jepesi kuliko mtu alieiba kuku.

Sababu ya hii hali inaweza kuwa ni watu kukataa tamaa na wanasiasa hasa wa upinzani.
 
Kweli kabisa, imechangia mpaka vipindi cya michezo kuongezeka na kupewa muda mwingi kwenye redio.
 
Hili suala mimi nilifikri ni peke yangu tu ndio naona!

Yani watz sasa hivi mada yao kubwa ni moja tu mpira basi.

Zamani tulikuwa tumezoea sisi wanaume ndio tunaojadili sana mambo ya mpira ila cha ajabu hata wanawake siku hizi mnatoka ngoma draw mkianza kubishania mpira.

Ndio maana sasa hivi kuna mambo mengi ya kijinga yanayopita huko selikali huwezi kuona yakiibuliwa na yeyote na hata akitokea mtu akiibua ufisadi sehemu watu wanachukulia poa tu. Mfano ni lile suala la mtu kujiunganishia bomba la mafuta yani lilikuwa jepesi kuliko mtu alieiiba kuku.

Sababu ya hii hali inaweza kuwa ni watu kukataa tamaa na wana siasa hasa wa upinzani.
Siasa ni stress tupu, watu wanaangalia burudani siyo vitu vya kutia stress... Kila siku kubishana Mbowe gaidi si gaidi... Mama anaupiga mwingi wengine mama Hana jipya. Ubishi tu usio na maana. Kwenye siasa watu wanachafuana lakini mpira watu wanajadili kama burudani
 
Kweli kabisa ,imechangia mpk vipindi cya michezo kuongezeka na kupewa muda mwingi kwenye redio .
[emoji23][emoji23][emoji23]Imagine watu toka saa 2 asubuhi hadi saa 8 mchana wanajadili mpira, alafu wanarudi tena saa 10 jioni kisha saa 3 usiku.
 
Mbona Mwijaku na Manara wanatukanana kwenye mpira?
Siasa ni stress tupu, watu wanaangalia burudani siyo vitu vya kutia stress... Kila siku kubishana Mbowe gaidi si gaidi... Mama anaupiga mwingi wengine mama Hana jipya. Ubishi tu usio na maana. Kwenye siasa watu wanachafuana lakini mpira watu wanajadili kama burudani
 
[emoji23][emoji23][emoji23]Imagine watu toka saa 2 asubuhi hadi saa 8 mchana wanajadili mpira, alafu wanarudi tena saa 10 jioni kisha saa 3 usiku.
Inasikitisha kwa kweli huko tunakoelekea,kwa utafiti usio rasmi nimegundua Tz ndio tunaongoza kwa mijadala ya kipuuzi .Hali imekuwa mbaya sana mipira mda wote tukipumzika ngono na wasanii ndo maana kupata vijana wenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja na hamasa chanya ktk jamii kama walivyokuwa wakina Nelson Mandela , Malcom X na wengine ni ngumu mno.
 
Hadi bosi au mkuu wa kitengo naye anabishana na sekretari wake wa kike kila siku kuhusu mauaji ya 'KIMBARI'yaliyotokea uwanja wa old Trafford siku chache zilizopita Kati ya Man United na Liverpool...Watu washawachoka wanasiasa uchwara ni hiyo Basi tu kuwa lazima uwanywe tu...
 
Kwanini serikali isianzishe task force ya makomandoo kutoka jeshini wawe wanatembea kuwasaka hao watu na kuwalazimisha kwenda kufanya kazi ama kuwapeleka kwa lazima kwenye mapori yetu lukuki yaliozagaa yapo yapo tu wayafyeke na wajishughulishe na kilimo?
Mkuu kulima sio rahisi kama unavyozungumza au unavyosikia kwa wapiga mbiu na soko lenyewe hata halieleweki..
 
Hili suala mimi nilifikri ni peke yangu tu ndio naona!

Yani watanzania sasa hivi mada yao kubwa ni moja tu mpira basi.

Zamani tulikuwa tumezoea sisi wanaume ndio tunaojadili sana mambo ya mpira ila cha ajabu hata wanawake siku hizi mnatoka ngoma draw mkianza kubishania mpira.

Ndio maana sasa hivi kuna mambo mengi ya kijinga yanayopita huko selikali huwezi kuona yakiibuliwa na yeyote na hata akitokea mtu akiibua ufisadi sehemu watu wanachukulia poa tu. Mfano ni lile suala la mtu kujiunganishia bomba la mafuta yaani lilikuwa jepesi kuliko mtu alieiba kuku.

Sababu ya hii hali inaweza kuwa ni watu kukataa tamaa na wanasiasa hasa wa upinzani.
Watanzania ni Mabingwa wa Ushabiki Mihemko wala hata siyo mpira.

Tengeneza chochote kile au TUKIO utaona kinavuna amashabiki wa kutosha tu.

Leo MATUKIO yana MASHABIKI,

Watu mitandaoni ni miungu watu, wana MASHABIKI lIALIA.

Wanasiasa wana MASHABIKI Lialia,

Influencers wana MASHABIKI LIALIA,

Media zina MASHABIKI Lialia,

Wanaharakati wana mashabiki LIALIA,

Na kUNA genge la watu wameshagundua hili, sasa hivi wamewekeza kwenye ADDICTION YA ushabiki HUU.

Huko Twiiter watu wanachangiwa pesa kwa mihemko tu wamefurahia,

wanasiasa wanapewa pesa bure bure tu,

Influencer wanatumia huo uraibu kupiga pesa,
 
2006 Hadi 2015 siasa ilitamalaki vichwani MWA watu na watu walikuwa commited kufatilia Bunge la bugte na siasa kiujumla hata kukosoa viongozi wao pale wanapokosea na wengi walihukumiwa kwenye sandulu la Kura, vijana wadogo walipewa nafasi na kuleta chachu kwenye ulingo WA siasa na walijitoa kufatilia na kutoa taarifa nyingi za ubadhirifu Ila Mambo yalikuja kubadilika kuanzia 2016 wanasiasa WA upinzani kurudi CCM na kibaya zaidi uchaguzi kufanyika bila kufata Sheria kibaya ziadi uchaguzi wa 2020 ndipo watu wakaona Bora ubet kuliko ufatilie siasa, na siasa ndyo maisha yetu ya kila siku, ajira hakuna Kwa vijana ukijiajiri shidaa au hakuna mazingira rafiki ya kujiajiri watu wenye mamlaka wanapiga pesa na hakuna WA kusema
 
Halafu sisi tofauti na mataifa mengine tunauzungumza na kuuchambua sana mpira lakini uwanjani timu zetu ni upupu mtupu.
Mchango mkubwa wa mpira katika nchi yetu ni betting sio viwanja vya kisasa, ajira kwa vijana wengi na academy za maana kwa vijana.
Kweli kabisa, imechangia mpaka vipindi cya michezo kuongezeka na kupewa muda mwingi kwenye redio.
 
Endeleeni kuburudika.

Back
Top Bottom