Kuna yoyote mwingine aliliona hili?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Wageni wengi waalikwa wakati wengine wakiwa wanaitwa mbele kumuapia Mungu wao na aliyewateua walikuwa tulivu kabisa lakini mara tu mteuliwaji mpya wa Idara ambayo ndiyo yenye Pesa kuliko zote nchini Tanzania ' Mwanamama ' mweupe kuliko wote waliowahi kuwa wateuliwaji wa Idara hapa nchini ' Wageni ' wengi waalikwa walianza Kuteta, Kunung'una, Kushikana mabegani hadi wengine wakisonteana japo kisirisiri na ni kama vile Wageni hao walikuwa na ' donge / dukuduku ' fulani hivi mioyoni mwao.

Je hili nimeliona tu peke yangu au kuna wale wenzangu tuliobarikiwa na macho ya ' Tai ' ya kuona yasiyoonekana kirahisi na Wao pia waliliona? Najiuliza maswali mengi sana ni kwanini huyu ' Mwanamama ' mweupe ' tiiiiiiiii ' alipoamka tu ndani mule ' pakachangamka ' na Wageni wengi ambao ndiyo walikuwa wakinong'ona, kuteta, kusonteana na kupiga majungu walikuwa ni wa Jinsia ya Kike japo kuna ' midume ' kadhaa nayo ilikuwa inafanya hivyo.

Siku zite wana JF hamjawahi kuniangusha kwa kila swali ninalowaulizeni hivyo ni matumaini yangu makubwa sana kwa hili nililolileta Kwenu na kwa jinsi ninavyowajua na kuwakubali kuwa nyie ni Great Thinkers wa uhakika hamtaniangusha ili nami pia niweze kujua na niwe Great Thinkers kama nyie.

Nawasilisha.
 
tuonyeshe ulivyoona
 
penye uvundo pana mzoga. ukipekua pekua nyasi utauona mzoga wenyewe, kama ni wa fisi au ni wa ng'ombe. na ukiona manyoya ujue keshaliwa hivyooooo. Ila si kila king'aacho ni dhahabu. kwa kumalizia, kwa wasukuma, mwanamke "mweupe" ni almasi. hutolewa mahari ya ng'ombe wengi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…