KING MIDAS
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 8,589
- 16,936
Kuna zile nyakati bhana… ndoa inazingua mno mno hadi unajiona wewe si kitu mbele za watu! Hata ukiwa kwa daladala unahisi wale abiria wenzio wote wanajua kile unapitia na ni kama wanakuzomea😂 Ni kipindi kigumu sana sana huzuni juu ya huzuni fanya ukisikie kwa jirani tu kisikukute!
Ni kipindi hicho hicho biashara inakufanya uongee peke yako yaani haisogei hadi unaaza kuona wachawi wamekuamulia! 😔😔
Afya nayo inazingua kunaibuka kiugonjwa hakieleweki mara miguu inawaka moto mara vidonda vya tumbo sijui vimekuwaje mweeee😭😭
Uchumi nao aiseeeee hata pesa ya panadol inagoma!
Madeni yamekuzonga na kukubadilishia jina unaanza kuitwa tapeli😂 Kama hujapita huwezi kuelewa my dear.
Marafiki wale mlifurahi pamoja wanaanza kusepa mmoja mmoja… ukiwapigia simu hawapokei na wakipokea ile pokea yao tu hata kueleza shida zako inakuwa ngumu! Sijui unanielewa?
Unaona acha niwatafute ndugu zangu😂😂 maana nina kakaangu ana pesa na yule dadaangu mambo yake si mabaya atanisaidia😉 Hehehe kile unakutana nacho kwa ndugu unabaki kuimba DUNIA HAINA HURUMA🤣🤣
Hakuna namna unabaki na Mungu peke yake… unaanza kuwa mtu wa maombi tu maana Mungu peke unaona ndiye mwenye kukupa amani!
Ni kakipindi karefu mno acha masihala…. Kagumu mno mno tena mno! Ila nikwambie sasa… ukivuka my kipenzi. Ukivuka hapo aiseeeee.
Kuna NEEMA inaachiliwa mpaka unaanza kujiona lastborn wa Mshua Yesu! Unaona namna anakudekeza mpaka unabaki 🥹🥹
Ila maisha acha tu!
Usiogope
Hautakufa
Hautaishia hapo…
Iko siku yataisha
Iko siku itabaki historia
Iko siku yako…
Mungu ni mwema sana kwetu!
Hayo unapita nayo ni Nyakati tu
Niamini kuna mahala unakwenda.
Kuna mahala unaelekea
Kuna Nchi yako iliyojaa maziwa na asali
Usiogope …
Utafika!
Jitie nguvu
Songa mbele
Kuna mahala unakwenda👌
Uwe na mapumziko mema ya mwisho wa juma.
Weekend Kareem🙏