KERO Kunani matengenezo ya barabara Getifonga-Mabogini-Kahe? Adha ya vumbi, vifusi, barabara hazipitiki na vifaa mmeondoa saiti. Tunataka maelezo

KERO Kunani matengenezo ya barabara Getifonga-Mabogini-Kahe? Adha ya vumbi, vifusi, barabara hazipitiki na vifaa mmeondoa saiti. Tunataka maelezo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Mkandarasi aliyepewa tenda ya kutengeneza barabara ya kilometa 31 ya Geti Fonga-Mabogini-Kahe wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro anasababisha kero kwa wakazi wa maeneo inapopita barabara hiyo. Mkandarasi huyo ni Lenana Holding Company Limited yenye makao makuu yake jijini Arusha.

Kero anayosababisha ni kwamba amechimba mitaro pembezoni mwa barabara lakini hakuna jambo linaloendelea. Vifusi vilivyokusanywa vinasababisha vumbi na makalvati yamezagaa kila mahali. Mitaro imechimbwa na kuzuia baadhi ya vipande vya barabara za mitaa zinazoingia barabara kuu kutopitika.

Mabo 11.jpg

Kifusi kilichotelekezwa zaidi ya miezi miwili

Ni muda mrefu sasa hata vifaa havipo site. Mara chache wanaonekana vijana fulani wakiwa na mabeleshi/chepe na majembe ya mkono wakitifua barabara. Hawa vijana hawajavaa vifaa vya usalama kazini kama inavyopaswa na hakuna dalili ya gari wanalofanya nalo kazi ni mali ya kampuni ya ujenzi. Hali hii inasababisha wananchi kupata mashaka kuwa huenda huyu mkandarasi anakodi vifaa ndiyo maana kuna kuchelewa kwa utekelezaji.

Itakuwa ni aibu kubwa kama Mkandarasi anaweza kupata tenda akiwa hana vifaa vya kisasa kufanya kazi hizi. Kumbe basi mtu yoyote tu anaweza kuwa na kampuni ya mfukoni na akapewa tenda ya kilomita 31, tena kwa mfuko wa libenki likubwa kabisa duniani. Aisee!

Vihana wa Mkandarasi.jpg

Vijana wa Mkandarasi wakitekeleza majukumu yao katika mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB).

"Huenda jamaa hawana vifaa vyao au wana tenda nyingi na vifaa vyao havitoshi, kwahiyo wanavisambaza maeneo mengi ili kuendelea kushikilia tenda. Kuna jambo halipo sawa na hatujui ni hadi lini tutaendelea kula hili vumbi", anasema mkazi mmoja ambaye pia ni mwendeshaji wa bodaboda.

Nilidhani ni mimi pekee niliyekuwa nikiona tatizo hilo kumbe linawakera watu wengi. Nilipohudhuria shughuli moja ya kijamii, kila aliyekuwa pale alikuwa akizungumzia mkandarasi huyo na adha ya vumbi, vifusi kila kona na mitaro mirefu ambayo haijakamilika.

Mabo 2.jpg

Cheki vumbi hilo!

TARURA wanajua kinachoendelea? Wanajua adha wanayopata wananchi? Mbona vifaa havipo katika eneo la matengenezo? Mamlaka za Mkoa zina taarifa na jambo hili au wanaona kwakuwa ni watu wa pembezoni mwa mji hawataweza kupaza sauti? Mbona hamna taarifa ya kinachoendelea? Au ni mradi ambao na "wakubwa" fulani wanahusika? Mradi unafadhiliwa na Benki ya Dunia; bado hawajatoa fungu la kumalizia kiporo kilichobaki?

Hayo ni baadhi tu ya maswali yetu watu wa huku Mabogini.

Hatutaki kuamini kuwa serikali imeleta huu mradi kimkakati tukielekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwasababu ni kilio chetu kwa muda mrefu sana. Vitendo vya mkandarasi na huenda baadhi ya watendaji wa serikali ngazi ya mkoa ndiyo wanaweza kusababisha tupate mashaka na serikali yetu.

Ni wito wetu kwa wizara husika, TARURA, na serikali ya mkoa kuhakikisha suala hili linapatiwa ufumbuzi.

Tukiwa na matarajio ya mvua hivi karibuni, tuna mashaka kazi italala tena hadi mvua zitakapoisha na hili litapelekea kuendelea kuchelewa kwa utekelezaji wake.

Picha nyinginezo:

Mabo 1.jpg

Mabo 3.jpg

Mabo 4.jpg
Mabo 5.jpg
Mabo 7.jpg

Mabo 6.jpg

Mabo 9.jpg

Mabo 10.jpg

Mkandarasi Mabo.jpg
 
Back
Top Bottom